Home VIWANDAMIUNDOMBINU Majaliwa aagiza NHC kuongeza nguvukazi ujenzi Dodoma

Majaliwa aagiza NHC kuongeza nguvukazi ujenzi Dodoma

0 comment 80 views

Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amemtaka Mkandarasi anayesimamia ujenzi wa ofisi mpya ya Wizara ya Fedha na Mipango kutoka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kuhakikisha anaongeza idadi ya watu katika mradi huo ili ujenzi ukamilike kwa wakati na katika viwango vya ubora unaotakiwa. Majaliwa ameagiza hayo wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa ofisi mbalimbali za wizara katika mji wa serikali Ihumwa jijini Dodoma.

Waziri amesisitiza kuwa zimesalia siku ishirini na moja pekee kukamilisha ujenzi huo na  lengo la serikali ni kuona kazi hiyo imekamilika hadi kufikia Januari 31 mwaka huu.

“Mimi ninapokuta watu wachache huku kukiwa na kazi zisizohitaji kusubiri siku mbili kama kazi ya kuweka bimu, natarajia kuona watu wangekuwa wanaendelea kufanya kazi hizo”. Amesema Waziri Mkuu Majaliwa.

Aidha, Majaliwa ameagiza Wizara ya Fedha na Mipango kwa kushirikiana na Wakala wa Misitu kuhakikisha mazingira ya eneo la wizara yanapandwa miti  kulingana na ramani ya majengo ya muda na ya kudumu.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter