Shirikisho la soka Tanzania (TFF) limetangaza mapato ya mechi ya Simba vs Yanga iliyochezwa Aprili 16 iliingiza Sh410 milioni.
Tarifa ya TFF imeeleza mgawanyo wa hela hizo ambapo VAT ni Sh62 milioni, Baraza la Michezo (BMT) Sh10 milioni, gharama za tiketi Sh22 milioni, uwanja Sh47 milioni na mchezo ni Sh22 milioni.
TFF imeeleza kuwa wao wamepata Sh12 milioni, Bodi ya Ligi Kuu Sh25 milioni, FA mkoa wa Dar Sh18 milioni.
“Katika mchezo huo jumla ya mashabiki 53,569 waliingia ambapo VIP A waliingia watazamaji 340 kwa kiingilio cha 30,000, VIP B watazamaji 4,160, VIP C watazamaji 2,004.
Jukwaa la rangi ya machungwa waliingiz watazamaji 10,372 na jukwaa la mzunguko watazamaji 36,693,” imesema taarifa hiyo.
Timu mwenyeji wa mchezo huo Simba imepata Sh188 milioni ambapo kwa mujibu wa kanuni timu mgeni kama ilivyo Yanga huwa haipati kitu.
Katika mchezo huo Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-0.