Home Elimu MAWAZILI SADC WAFANYA MKUTANO JIJINI DAR ES SALAAM.

MAWAZILI SADC WAFANYA MKUTANO JIJINI DAR ES SALAAM.

0 comment 38 views

Mkutano wa Mawaziri wa Kamati ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ya Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama kwa ngazi ya Makatibu Wakuu/ Maafisa Waandamizi umefanyika tarehe 25 Juni,2020, Jijini Dar es Salaam kwa njia ya Mtandao (Video Conferencing).

Mhimili wa Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC unaongozwa na mfumo wa Utatu (Troika) ambapo kwa sasa Mwenyekiti ni Zimbabwe, mkutano wa ngazi ya Makatibu Wakuu unaofanyika leo ni maandalizi ya mkutano wa Mawaziri utakaofanyika tarehe 26 Juni 2020 chini ya Uenyekiti wa Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara ya Kimataifa wa Jamhuri ya Zimbabwe, Mhe. Sibusiso Busi Moyo na utakutanisha Mawaziri wenye dhamana ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mambo ya Ndani, Ulinzi na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama kutoka nchi wanachama wa SADC.

Pamoja na mambo mengine mkutano umepokea na kujadili agenda zinazohusu masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama katika Ukanda wa SADC.Mkutano wa leo umehudhuriwa na nchi wanachama wa SADC ambazo ni Angola, Afrika Kusini, Botswana, DRC, Eswatini, Lesotho, Malawi, Mauritius, Msumbiji, Madagascar, Namibia, Zambia, Zimbabwe na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC ni moja ya mihimili ya SADC inayosimamia masuala ya Usirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama katika Kanda. Mhimili huu unatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia Mkataba wa uanzishwaji wa SADC wa mwaka 1992 na Itifaki ya Asasi ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC ya mwaka 2001.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter