Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKIBIASHARA Umuhimu wa biashara kuwekeza kwenye amani

Umuhimu wa biashara kuwekeza kwenye amani

0 comment 164 views
  • Ukuzaji amani katika enzi za dijitali

Amani inapovunjika, ni jamii ya kawaida na biashara zinazo umia sana. Uchumi huporomoka pasipo na amani.

Hivio, kuna haja ya biashara kuchukua hatua madhubuti kukuza na kuwezesha amani hasa sasa, katika kipindi hiki ambacho mitandao ya kijamii inatumika kueneza uchochezi. Mitandao ya kijami inaweza kutumika kuzuia mizozo na uenezi wa msimamo mkali na badala yake kukuza uelewa na uvumilivu.

“Lazima tuchukue hatua kuhakikisha tunapanda mbegu za amani na uvumilivu kwa kila mmoja, na mitandao ya kijamii ni jukwaa zuri la kufikia vijana ,” alisema Martha Nghambi, Mkurugenzi wa Global Peace Foundation Tanzania.

Akiongea na wanahabari mwanzo wa wiki, alitangaza kwamba GPLC itafanya mkutano wa  mtandaoni Julai (30-31) kujadili mbinu mbali mbali za kukuza amani.

“Mkutano huo ulipangwa kufanyiwa Nairobi lakini kwa vile nchi nyingi bado zinaendelea kuchukua taadhari zidi ya Covid-19, badala yake mkutano utafanyiwa mtandaoni,” alisema.

Mkutano huu unafuatia mkutano wa mwisho uliofanywa nchini Uganda na kusimamiwa na mgeni rasmi raisi Yoweri Kaguta Museveni.

Mkutano huo ulikusanya zaidi ya wajumbe 1000 wakiwemo viongozi mbali mbali. Hotuba ya Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ilisomwa na Katibu wa Baraza la Mawaziri Mhe. Eugene Wamalwa na ya rais wa Tanzania John Magufuli ilisomwa na aliekuwa Waziri wa Katiba na Sheria Mheshiwa Augustine Mahiga.

Akiendelea kuzungumza na waandishi, Nghambi  alisisitiza umuhimu wa ushiriki wa vijana kama wanufaika wa moja kwa moja.

“Kuwashirikisha vijana kunawafanya kuwa watetezi na pia inawapa nguvu kuchukua hatua badala ya kutumiwa kuwa wachochezi,” alisema.

Zaidi, “… tunao mradi unaoendelea unaoitwa ‘Wanawake Sasa’ ambao unalenga kuwezesha wanawake vijana katika uongozi bora, kuzuia migogoro, kukuza amani kabla ya na baada ya chaguzi kuu.”

Kwa sasa, GPLC pia inaendesha kampeni ya Vijana na Amani inayo wahamasisha vijana kuwana maadili, ujuzi, stadi za kazi na mbinu za kuzuia uvunjaji wa amani.

Lengo kuu la kampeni hii ni kuwapa vijana nguvu kuwa chachu ya maendeleo na kuwapa utambuzi chanya iliwawe chanzo cha jamii zenye amani.

GPLC ni jukwa linalo kusanya viongozi kutoka serikalini, wafanya biashara, wasomi, mashirika ya sio ya kiserekali  na taasisi za kidini kubadilishana mitazamo juu ya uongozi bora katika jamii. Mkutano huu ni wa 10 tangu ‘Mkutano wa Amani wa Dunia wa 2010’ uliofanyika jijini Nairobi chini ya rais mtsaafu Mwai Kibaki.

GPLC ya mwaka huu itabainisha uzoefu wa Kenya kulinda ustawi wa amani kwenye Pembe ya Afrika ikiwemo juhudi zake kusimamia utulivu wa amani Somali, Sudani, na Sudani Kusini. Mkutano huu pia, utatambua juhudi za Rais Uhuru Kenyatta kukuza ushirikiano wa kimataifa na maridhiano baina ya Kenya na nchi zingine za Pembe ya Afrika.

Maridhiano haya yalianzishwa na aliekuwa Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga ambao umekuwa mfano wa kutafuta suluhisho za matitizo ya kisiasa.

Kati ya mada kuu za mkutano huu ni kubadilisha uboreshaji wa maadili ya uongozi na ubunifu, kujenga umoja wa kijamii, tabia, mikakati ya ubunifu wa utekelezaji wa elimu na kujenga ujasiri wa vijana kusimamia amani katika enzi za dijitali.

Ulimwengu unabadilika haraka na kwa njia zisizotabirika. Waelimishaji na wasimamizi wanahitaji kufikiria tena njia ambazo wanaweza kuandaa kizazi kijacho kwa siku zijazo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter