Home VIWANDAUZALISHAJI Mapato sekta ya madini yaongezeka

Mapato sekta ya madini yaongezeka

0 comment 77 views

Serikali imesema mpango wake ni kuhakikisha kuwa sekta ya madini inachangia asilimia 10 au zaidi katika Pato la Taifa ifikapo 2025.

Ukuaji wa Sekta ya Madini umeongezeka kutoka asilimia 9.4 Mwaka 2021 hadi kufikia asilimia 11.3 Mwaka 2023 kutokana na kuendelea kuimarika kwa Sekta, Mchango wa Sekta ya Madini katika Pato la Taifa utaongezeka na kufikia asilimia 10 au zaidi ifikapo Mwaka 2025 kama ilivyoelezwa katika Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025.

“Serikali imefanya uwekezaji mkubwa katika Sekta ya Madini, tumenunua mitambo mikubwa, mitano imeshafika nchini, kumi ipo njiani inakuja, mitambo hii itawarahisishia wachimbaji wadogo kupata taarifa za uchimbaji na kuwaepusha na hasara,” kauli ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, aliyoitoa Oktoba 21, 2024 ambapo aliongeza,

“Mitambo hii ikifika itagawanywa pote, ila nimemtaka Waziri (Anthony Mavunde) atenge mitambo miwili kwa ajili ya vijana na mmoja kwa ajili ya wanawake.

Kauli hiyo ya Rais Samia ni muendelezo wa dhamira yake ya dhati ya kuhakikisha Sekta ya Madini inaendelea kuongeza mchango wake katika ukuaji wa uchumi wa nchi.

Uboreshaji wa sheria, kanuni na miundombinu ikiwemo ya umeme migodini, ndani ya miaka mitatu ya Rais Samia Suluhu Hassan, kupitia Tume ya Madini kiwango cha makusanyo ya maduhuli ya Serikali kimepanda kutoka Shilingi bilioni 624.61 zilizokusanywa Mwaka wa Fedha 2021/2022 hadi kufikia Shilingi bilioni 753.82 Mwaka wa Fedha 2023/2024, makusanyo hayo ni sawa na ongezeko la asilimia 20.7 ya makusanyo kwa miaka mitatu.

Mhandisi Ramadhani Lwamo, Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini hivi karibuni katika kikao chake na Wahariri wa Vyombo vya Habari amesema “mathalani katika kipindi cha mwaka wa fedha 2024/2025 ambapo tulipewa lengo la kukusanya shilingi Trilioni Moja, hadi kufikia Oktoba 21, 2024 Tume ya Madini imefanikiwa kukusanya Jumla ya Shilingi bilioni 312.75 sawa na asilimia 31.28 ya lengo la mwaka.”

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter