Home VIWANDA Serikali yatoa neno sakata la saruji

Serikali yatoa neno sakata la saruji

0 comment 125 views

Serikali kupitia Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji imekutana na wadau wa sekta ya viwanda kujadili kuadimika kwa saruji, sambamba na kupanda bei kwa bidhaa hiyo ambayo imeadimika sokoni. Akiongoza kikao hicho Naibu Waziri wa wizara hiyo Mhandisi Stella Manyanya pamoja na wazalishaji wa saruji, makaa ya mawe pamoja na wasafirishaji na wadhibiti wamejadili sababu za kupungua kwa uzalishaji na kusimamishwa uzalishaji kwa baadhi ya viwanda hivyo. Waziri Manyanya pia amewataka wazalishaji wa saruji kueleza uwezo wa uzalishaji wa bidhaa hiyo kwa kila kiwanda.

“Imenishtua kuwa saruji imepotea sokoni na kupanda bei ghafla, tena viwanda vyote. Tukasema hapo ni zaidi ya masuala ya kiufundi, kwa hiyo tumewaita kuwasilikiliza tujue tatizo ni nini ikiwezekana leo tutoke na uamuzi”.  Amesema Manyanya.

Waziri Manyanya amesema kuwa kipindi hiki kuna fursa nyingi za soko la saruji lakini ameshangazwa kuona bidhaa hiyo ikipotea sokoni na kupanda bei ghafla. Bidhaa ya saruji imepanda bei kutoka Sh. 13,000 kwa mfuko na kufikia Sh. 18,000 hadi Sh. 20,000 kulingana na maeneo.

Naye Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage ameeleza sababu zinazopelekea kuadimika kwa saruji nchini na kutaja ubovu wa miundombinu katika kiwanda cha Simba Cement na kuharibika kwa mtambo wa uzalishaji katika kiwanda cha Dangote ambao ni wazalishaji wakubwa kupelekea tatizo hilo kwa kiasi kikubwa.

Hata hivyo, ukarabati katika kiwanda cha Twiga Cement unaendelea kutokana na uzalishaji mkubwa uliofanyika hivi karibuni kutokana na uhitaji wa serikali katika ujenzi na ukarabati wa miradi mbalimbali nchini.  Waziri Mwijage amesema changamoto hiyo itaisha hivi karibuni kwa sababu mzalishaji mkuu ambaye ni kiwanda cha Dangote wameanza uzalishaji mwezi Julai baada ya kufanyiwa matengenezo.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter