Home BIASHARA Mwijage asikia kilio cha wafanyabiashara

Mwijage asikia kilio cha wafanyabiashara

0 comment 40 views

 

Waziri wa Viwanda, Biashara naUwekezaji, Charles Mwijage amewaagiza viongozi mkoani Mara kuandaa jukwaa maalumu kwa ajili ya wafanyabiashara na mifuko ya taifa ya uwezeshaji uchumi. Mwijage ametoa agizo hilo akiwa mkoani Mara baada ya kupokea malalamiko ya wafanyabiashara kuhusu kutonufaika na fursa ya uwepo mifuko na taasisi za uwezeshaji kiuchumi ikiwa ni matokeo ya ukosefu wa ofisi za mifuko hiyo mkoani humo.

“Mkutano huo wa jukwaa la uchumi ufanyike ifikapo au kabla ya Desemba ili kuwawezesha wafanyabishara wa mkoa huu kunufaika kutokana na mifuko ya uwezeshaji”. Alisema Mwijage.

Agizo hilo limetolewa na Waziri Mwijage ikiwa ni matokeo ya hoja iliyotolewa na kuwasilishwa na Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara wa Viwanda na Kilimo (TCCIA) mkoani Mara Boniface Ndengo akihoji kuhusu wajasiriamali, wafanyabiashara wakubwa na wadogo kukosa mikopo licha ya uwepo wa taasisi na mifuko ya uwezeshaji.

“Wachache waliopata mikopo kutoka taasisi hii walilazimika kufuata huduma hii jijini Mwanza, Dodoma au Dar es salaam ziliko ofisi za taasisi na mifuko hiyo”. Amesema Ndengo.

Aidha Mwenyekiti huyo amesema kuwa uhaba wa matawi ya Benki ya uwezeshaji (TIB) na Benki ya wakulima (TADB) mkoani humo yanakwamisha maendeleo ya sekta ya Kilimo na ufugaji licha ya mkoa huo kuwa na ardhi nzuri na yenye rutuba.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter