Home VIWANDA Majaliwa:Viwanda vimepunguza changamoto ya ajira

Majaliwa:Viwanda vimepunguza changamoto ya ajira

0 comment 130 views

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema kwa kiasi kikubwa kuanza kufanya kazi kwa viwanda vingi hapa nchini kumesaidia kutatua changamoto ya upatikanaji wa ajira hususani kwa vijana. Majaliwa amesema hayo alipotembelea kiwanda cha kukoboa kahawa cha BUKOP na kile cha kusindika kahawa cha Tanica, ambapo ameeleza kuwa, kwa sasa vitendo vya vijana wengi kukaa vijiweni vimepungua baada ya wengi kuajiriwa katika viwanda mbalimbali vilivyoanzishwa na kufufuliwa ambapo ameongeza kuwa viwanda vimekuwa vikitoa ajira nyingi kwa wananchi huku alitolea mfano kiwanda cha Tanica kilichoajiri watumishi 800.

“Nyie mlioajiriwa kiwandani hapa hakikishe mnafanya kazi kwa bidii, weledi, uaminifu na uadilifu wa hali ya juu ili kukiwezesha kiwanda kuendelea na uzalishaji”. Amesema Waziri Mkuu.

Majaliwa ambaye yuko mkoani Kagera kwa ziara ya siku nne maalum kwa ajili ya kufuatilia maendeleo ya viwanda na zao la kahawa pia amemuagiza Mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Bukoba, Bernad Limbe kuhakikisha wafanyabiashara wadogo wanapatiwa eneo ili kuendesha shughuli zao bila uonevu wowote.

Kwa upande wake, Meneja Mkuu wa kiwanda cha Tanica, Linus Leopord amesema kwa mwaka, wanazalisha takribani tani 600 za kahawa iliyokaangwa na kusagwa, ambayo inatosheleza kwa mahitaji ya soko. Kiwanda hicho pia kina uwezo wa kuzalisha kahawa ya unga tani 500 kwa mwaka lakini kutokana na kuchakaa kwa miundombinu, kinazalisha tani 300 pekee kwa mwaka.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter