Home VIWANDANISHATI TANESCO yakusanya mabilioni Arusha

TANESCO yakusanya mabilioni Arusha

0 comment 119 views

Meneja wa Shirika la umeme (TANESCO) mkoani Arusha Mhandisi Herinia waandishi wa habari kuwa, shirika hilo linakusanya takribani Sh. 9.7 bilioni kwa mwezi na kuongeza kuwa wamejipanga kuhakikisha wanaongeza zaidi wigo wa ukusanyaji mapato. Mhandisi Mhina amesema japokuwa kuna changamoto mbalimbali wanazopitia, shirika hilo limejipanga kutoa huduma bora ya umeme wa uhakika kwa wananchi Meneja huto ameeleza kuwa TANESCO inaendelea na mchakato wa kuwafikia na kuwaunganisha wateja na huduma za umeme huku wakiwa wamejipanga kuhakikisha kila anayehitaji huduma hiyo anafikiwa pasipo vikwazo.

 

“Shirika letu limejipanga kuhakikisha wateja wanafikiwa na umeme kwa gharama nafuu kwa kila atakayelipia atafungiwa umeme bila kuchelewa tena kwa wakati na tumejipanga kuondoa kero ambazo wateja wamekuwa wakikumbana nazo”. Amesema Mhandisi Mhina.

 

Vilevile, Meneja huyo ameeleza kuwa hadi sasa, TANESCO imefanikiwa kuwaunganishia umeme wateja 142.310 mkoani humo na wanaendelea kusogeza huduma ya umeme hadi vijijini kupitia mradi wa umeme vijijini awamu ya tatu (REA III).

 

“Nawasihi wale wote wanaohitaji kupata huduma ya umeme wafike ofisi za shirika na kuacha kukutana na vishoka ambao wamekuwa ni kikwazo kikubwa cha kuongeza wateja na kuzidi kwa vitendo vya wizi wa umeme kwa wananchi”. Amesisitiza Mhandisi huyo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter