Home Uncategorized Jinsi Uhalifu wa kimtandao unavyohujumu uchumi.

Jinsi Uhalifu wa kimtandao unavyohujumu uchumi.

0 comment 100 views

Licha ya faida chanya za maendeleo ya sayansi na teknolojia ambayo hubadilika kila siku pia tumeshuhudia mabadiliko haya yakiambatana na vitu hasi ambavyo hatukuwahi kuviwaza hapo kabla ikiwemo kuongezeka kwa kasi kwa wimbi la uhalifu hasa wa kimtandao(cyber crimes).

Kiufupi uhalifu wa kimtandao ni aina mpya ya uhalifu ambayo inahusisha matumizi mabaya ya mitandao kwa kutoa taarifa ambazo si za ukweli zenye lengo la kufanya uhalifu ikiwemo wizi,utapeli kwa kutumia simu,kompyuta au mtandao wa intaneti.

Nchi nyingi duniani zimeathirika na aina hii ya wizi hasa nchi za amerika,ulaya na afrika ambapo nchi kama Nigeria na afrika kusini zimeathirika zaidi.

Kwa upande wa Afrika mashariki Tanzania pia ni mhanga wa uhalifu huu wa mitandao ambapo inakadiriwa watu zaidi ya milioni 7 wanaotumia intaneti huku zaidi ya watu milioni 40 wakitumia simu za mkononi,kesi kadhaa zimeripotiwa huku zingine zikiwa mikononi na vyombo vya sheria kwa ajili ya kukamilisha taratibu kabla ya wahusika kuhukumiwa.

Uhalifu huu umekua na athari katika uchumi wa nchi nyingi ikiwemo Tanzania ambapo athari mbalimbali zimeripotiwa ikiwemo upotevu wa mapato kwa nchi kwani fedha hizi zingeingizwa katika mzunguko wa kawaida nchi ingepata mapato kutokana na kodi mbalimbali kama kodi ya ongezeko la thamani (vat) pia kodi za huduma mbalimbali ambazo zingepatikana kupita matumizi halali ya fedha hizi.Takwimu zinaonyesha Tanzania imepoteza zaidi ya 187 bilioni kwa njia ya miamala iliyofanyika kwa njia ya simu(AIPC)

Pia uhalifu wa mitandao umepelekea anguko la biashara nyingi hasa zile ndogondogo za miamala ya fedha ambapo raia wengi wamepoteza ajira na vipato kutokana wimbi hili la wizi.Kufa kwa biashara hizi kumepunguza mzunguko wa fedha katika maeneo husika hivyo kusababisha kudorora kwa uchumi.

Usumbufu kwa wahusika pia ni athari nyingine inayowakumba wahanga wa aina hii ya wizi ambapo hutumia muda mrefu kushughulikia taratibu za kisheria na mahakama hivyo kupoteza nguvu kazi ambayo ingeelekezwa katika kuinua uchumi wa wahusika na nchi kwa ujumla.

Kuongezeka kwa vitendo vya utakatishaji fedha(money laundering),Wizi wa kimtandao wahusika hupata fedha kwa njia ambayo siyo halali hivyo huitaji kuitakatisha fedha hiyo ili kuingiza katika mzunguko ambao ni halali ili waweze kufanya matumizi ya kawaida.Utakatishaji fedha ni sumu katika kukua kwa uchumi maana husababisha mzunguko wa fedha usio halali hivyo kushusha thamani ya fedha husika.Nchi yenye wimbi kubwa la utakatishaji fedha hukabiliwa na tatizo kubwa la kukua kwa uchumi.

Kuongezeka kwa Makosa ya uhujumu uchumi(Economic crimes) uhalifu wa kimtandao hugusa sekta mbalimbali zikiwemo taasisi za serikali hivyo kuikosesha serikali mapato kwa namna moja ama nyingine.Moja ya athari kubwa ya uhalifu huu ni ukwepaji wa kodi ambao huinyima serikali mapato kutokana na hujuma zinazofanyika zenye lengo la kutoa taarifa za uongo kwa njia ya kimtandao ili wahusika wapate fedha kinyume na taratibu.

NINI KIFANYIKE?

Elimu kwa wananchi kuhusu aina hii ya uhalifu lazima itolewe kwa wingi ikielezea mbinu zinazotumika na jinsi ya kuepuka kutoa taarifa za siri za akaunti za muhusika kwa mtu yeyote.

Pia Wananchi wahimizwe kuhusu kuwa wazalendo kwa nchi yao ili kuepuka hujuma kwa kuinyima nchi mapato,Elimu juu ya madhara ya uhujumu uchumi lazima itolewe kwa wananchi husika.

Kudhibiti uingiaji wa wananchi kiholela nchini kwa kuhakika kila raia wa kigeni anafata taratibu husika na kuwa na vibali husika vya shughuli ambayo anaifanya ili kuepuka uchumi wa nchi kuhujumiwa na raia ambao sio wazalendo.

Mamlaka husika zinazozimamia na kudhibiti shughuli za mitandao kama vile TCRA lazima zisimame imara katika kudhibiti aina hii ya uhalifu kwa kuhakikisha wahusika wanafikishwa mahakamani kwa makosa mbalimbali ikiwemo kuhujumu uchumi wan chi na uhalifu wa mtandao.Pia mamlaka za rushwa(Takukuru) zisimame imara kuhakisha vitendo vya rushwa vinakomeshwa ili kudhibiti aina hii ya wizi ambayo inahusisha rushwa ndani yake.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter