Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKIUJASIRIAMALI Unachohitaji kutimiza malengo yako

Unachohitaji kutimiza malengo yako

0 comment 105 views

Ili kufanikiwa kama mjasiriamali, unatakiwa kujiwekea malengo ambayo yatakuwezesha kufika pale unapotaka. Biashara sio tu kuwa na mpango wa biashara. Malengo ni muhimu kwa kuwa yanakuwezesha kupiga hatua na kufika mbali zaidi.

Wakati unaweka mipango hii sawa, ni muhimu kuzingatia yafuatayo:

  • Tathmini nini hasa unataka kutimiza. Upo katika nafasi nzuri zaidi ya kufanikiwa kama unafahamu ni nini hasa unataka. Mipango yako inatakiwa kuwa katika mstari ulionyooka na unatakiwa kujua lengo lako ni nini. Kutafuta mtaji kwa mfano, sio lengo lakini kutafuta Sh. 100,000 ndani ya mwezi mmoja ni lengo ambalo unaweza kuwekeza jitihada zako  na kulitimiza. Kama mjasiriamali, ni vyema kujiuliza lengo lako maalum ni lipi? Usiweke malengo tu, weka malengo ambayo yatakuhamasisha kutimiza na hivyo kukuza biashara yako
  • Malengo yako yaendane na mazingira halisi: Kama unaweka lengo la kuingiza Sh. 1,000,000 kwa mwezi japokuwa hujaingiza kiasi hicho cha fedha mwaka mzima, itakuwa ngumu kutimiza. Katika hatua za mwanzo, jiwekee malengo madogo yaliyo ndani ya uwezo wako. Kwa mfano, unaweza kuongeza mapato yako ya mwezi kwa asilimia 25. Kama unaweza kutimiza lengo hilo, basi unaweza kupandisha kwenda kiwango cha juu zaidi kadri siku zinavyokwenda. Malengo unayojiwekea yanatakiwa kwenda sambamba na uhalisia wa biashara yako.
  • Weka mipango ya muda mfupi na mrefu: Kufanya hivi kunasaidia kuona maendeleo yako ya wiki, mwezi na mwaka na vilevile yatakusaidia wewe kama mfanyabiashara kujua nini hasa unataka ndani ya wiki, mwezi, miezi sita au mwaka mmoja. Mipango yako ya muda mrefu inaweza kuwa kati ya miaka mitano hadi 10. Unaweza kutathmini jitihada za kutimiza malengo yako ya muda mrefu kutokana na kile unachofanya kwenye malengo yako ya muda mfupi. Vitu hivi viwili hutegemeana hivyo ukifanikiwa upande mmoja umefanikiwa pande zote mbili.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter