Home VIWANDA Teknolojia ya kusaga chupa kuinua ujasiriamali Kilimanjaro

Teknolojia ya kusaga chupa kuinua ujasiriamali Kilimanjaro

0 comment 161 views
Na Mwandishi wetu

Meneja wa Shirika la kuhudumia viwanda vidogo vidogo (SIDO) Mkoa wa Kilimanjaro Hamweli Meena amesema kuwa ugunduzi wa teknolojia ya mashine za kisasa za kusaga chupa za plastiki na kubadili taka kuwa malighafi kwa viwanda hapa nchini itazalisha ajira za ukusanyaji wa chupa za plastiki na hivyo kuongeza idadi ya viwanda vidogo.

Arthur Ndedya, Meneja wa kitengo cha TDC ambacho husimamia Maendeleo ya teknolojia akielezea kwa undani juu ya ugunduzi huo amesema gharama za mashine moja inafikia zaidi ya Sh 4.5 milioni hivyo wajasiriamali wadogo wanaweza kununua na kuzitumia ili kujiajiri.

Mbali na hayo, Meya wa Manispaa ya Moshi, Raymond Mboya amesema kuwa teknolojia hiyo mbali na kuwezesha wananchi kwenye masuala ya ujasiriamali, itasaidia kudumisha usafi katika manispaa hiyo.

Katika mashindano ya usafi wa mazingira kwa mwaka 2017 ambayo yalishirikisha halmashauri 185 yakiwemo majiji  manne, manispaa ishirini na moja, miji ishirini na moja na halmashauri za wilaya ishirini na saba Manispaa ya Moshi iliibuka kidedea kwa kupata asilimia 78.5

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter