Home BENKI Kicheko tupu sekta ya benki

Kicheko tupu sekta ya benki

0 comment 146 views

Sekta ya benki imeonyesha neema katika robo ya pili ya mwaka huu ambapo kwa mujibu wa taarifa ya fedha iliyotolewa, benki nyingi zimeonyesha ongezeko la amana pamoja na mali.

 

Kwa maelezo ya taarifa hiyo, mali za Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) zimeongezeka kwa asilimia 6.6 huku amana za wateja zikiongezeka kwa asilimia 9.7 na kufikia Sh. 1.37 trilioni. Kwa upande wa Benki ya CRDB, mali zake zimeongezeka na kufikia Sh. 5.92 trilioni kutoka Sh. 5.89 trilioni ya robo ya kwanza. Amana za wateja nazo zimeongezeka na kufikia Sh. 4.33 trilioni.

 

Vilevile katika taarifa hiyo, benki nyingine ambazo ia zimefanya vziuri ni pamoja na Standard Chartered, Mkombozi, NIC, Benki ya Posta (TPB), Yetu Microfinance, I&M, Equity, Azania; Barclays, Benki ya Biashara ya Afrika pamoja na Amana.

 

Pamoja na benki nyingi kuonyesha mafanikio, nyingine kama Ecobank, First National Bank (FNM) na Benki ya Maendeleo zimeonyesha upungufu wa mali na amana za wateja.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter