Home BIASHARABIASHARA NDOGO NDOGO Makonda atoa wiki moja utoaji vitambulisho

Makonda atoa wiki moja utoaji vitambulisho

0 comment 121 views

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ametoa muda wa siku saba wakuu wa wilaya za Kigamboni, Kinondoni, na Ubungo kukamilisha mchakato wa kutoa vitambulisho kwa wajasiriamali.

“Nataka wamachinga wote wapate vitambulisho na isitokee watu waendeshe shughuli zao bila vitambulisho. Vitambulisho hivi ni kwa mwaka mmoja tukichelewa kugawa kwa wakati matokeo yake mwakani tutapata shida nyingine. Naomba waongeze kasi ya kuwasimamia watendaji wao kila mtaa na kata vitambulisho vimefika kabla ya mwisho wa wiki sitaki kusikia habari ya vitambulisho bali ibakie suala la kusimamia Sheria”. Amesema Makonda.

Kutokana na idadi ya watu, RC Makonda amesema jiji la Dar es salaam limepatiwa vitambulisho takribani 175,000 ambapo wilaya za Ubungo, Kinondoni, Temeke na Ilala walipewa vitambulisho 37,000 na kwa upande wa Kigamboni, walipewa jumla ya vitambulisho 27,000.

Wakati huo huo, Makonda amepongeza ufanisi wa Sophia Mjema na Felix Lyaniva (wakuu wa wilaya za Ilala na Temeke) kwenye zoezi la kugawa vitambulisho hivyo kwa wafanyabiashara wadogo.

 

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter