Home FEDHA Mbunge aomba madiwani kuongezewa posho

Mbunge aomba madiwani kuongezewa posho

0 comment 116 views

Mbunge wa Muheza, Adadi Rajabu ametoa wito kwa serikali kuongeza posho kwa madiwani kwa kuwa mchango wao katika kuchochea maendeleo miongoni mwa wananchi ni mkubwa. Mbunge huyo amesema hayo bungeni Dodoma alipokuwa akichangia hotuba ya bajeti ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Utawala Bora na Utumishi kwa mwaka wa fedha 2019/2020.

“Hawa ni viongozi muhimu sana katika utendaji kazi wa serikali na ndiyo walio jirani na wananchi, kwa hiyo, kuna haja serikali iwalipe posho kwa sababu kufanya hivyo ni njia mojawapo ya kuwapa moyo wa kutimiza majukumu yao ya kila siku”. Amesema Rajabu.

Mbunge huyo ameeleza kuwa kuna kila sababu ya posho za madiwani kuandaliwa kwa umakini ili waendelee kutekeleza majukumu yao kwa weledi.  Akizungumzia miradi ya kimkakati, Rajabu ameomba serikali kuipatia Halmashauri ya Muheza fedha kwa ajili ya utekelezaji wa ujenzi wa stendi kubwa ya kisasa.

Kwa upande wake, Mbunge Daniel Mtuka wa Manyoni ameitaka serikali kuangalia uwezekano wa kuongeza bajeti ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kutokana na taasisi hiyo kuwa na majukumu mengi.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter