Home FEDHA Punguza gharama kwa kufanya haya

Punguza gharama kwa kufanya haya

0 comment 93 views

Ili kupata mafanikio katika kampuni ni muhimu kuhakikisha kuwa gharama za matumizi na uzalishaji ni ndogo ili kuweza kutengeneza faida zaidi. Pia kuna kipindi kampuni inaweza kuwa inapitia changamoto za kifedha hivyo ili kuepuka kuathirika ni vyema kuchukua hatua ambazo zitasaidia kuendesha kampuni licha ya changamoto zinazotokea katika muda huo.

Yafuatayo ni baadhi ya mambo ambayo yanaweza kufanyika ili kupunguza gharama za matumizi katika kampuni.

Pitia gharama za uzalishaji kisha tafuta njia mbadala kuzipunguza. Hapa ni muhimu kuangalia mchakato mzima wa uzalishaji ili kutambua mambo ambayo yanatumia fedha nyingi zaidi kisha kutenga mpango mpya wa kutafuta njia mbadala ambazo ni nafuu zaidi. Kwa mfano kama kampuni inatumia umeme mwingi kufanya uzalishaji basi inaweza kuachana na nishati hiyo na kutumia nishati mbadala kama gesi asilia ambayo ni bei rafiki zaidi.

Tumia teknolojia kurahisisha ufanisi wa kazi. Lengo la teknolojia ni kurahisisha kazi na kampuni nyingi zimeokoa fedha kupitia mifumo mbalimbali ya kisasa. Moja ya mambo ambayo yanaweza kufanyika kwa teknolojia na kuokoa fedha ni pamoja na kufanya vikao kwa kutumia programu zinazopatikana katika kompyuta kwa mfano Skype. Pia watu wengi wamenufaika zaidi kwa kutumia mitandao ya kijamii kujitangaza na kuuza bidhaa au huduma zao badala ya kujitangaza katika mifumo ya matangazo kupitia televisheni, redio na magazeti ambayo ni gharama.

Fanya biashara kupitia mitandao. Inaweza kufikia kipindi unakosa hadi fedha ya kodi kwa ajili ya kampuni yako. Hivyo ili kupunguza unaweza kufanya biashara yako kwa njia ya mtandao. Jambo la msingi ni kuwa wazi kwa wateja kuwa unapatikana (Online) na ikiwa inahitajika kufanya mikutano ya ana kwa ana na aidha wateja au wawekezaji basi si vibaya kutumia programu kama ‘Worknasi’ ili kuhakikisha kila michakato ya kazi inakwenda sawa.

Pia unaweza kutafuta watoa huduma wa bei nafuu. Siku hizi uwepo wa teknolojia na mtandao umerahisisha mambo mengi. Ni rahisi kuangalia watoa huduma hata kupitia mtandao na kutafuta wanaoendana na bajeti uliyonayo. Hivyo fanya maamuzi sahihi ili kuokoa mtiririko wa fedha katika kampuni kama mambo hayapo sawa na hata yakiwa sawa. Mbali na hayo, unaweza kutoa likizo zisizo na malipo kwa wafanyakazi ikiwa unaona gharama zimezidi. Hii itakusaidia kuelekeza fedha katika mambo mengine ambayo yanaweza kuzalisha fedha zaidi.

 

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter