Wizara ya afya nchini Tanzania imethibitisha kuwa watu 84 wapya wameambukizwa virusi vya corona na kufikisha idadi ya wagonjwa wa Covid-19 kufikia 254.
Wagonjwa hao wanatoka katika pande zote mbili za Tanzania, Zanzibar.
Kwa upande wa Bara maambukizi ya virusi hivyo sasa yameripotiwa katika mikoa 17, na wagonjwa wapya waliotangazwa Jumanne na Waziri Ummy mwalimu wanatoka mikoa ya Dar es Salaam(33), Arusha (4),Mbeya(3), Dodoma (3), Kilimanjaro(3), Pwani,(3) Tanga(3), Manyara(2), Tabora(1), Ruvuma(2), Morogoro(2) Rukwa(2), Kagera(1), Mara(1) na Lindi (1).
Habari zaidi zilizotolewa Jumatatu jioni na wizara hiyo zinaarifu kuwa watu watatu wapya wamefariki kutokana na sababu zinazohusiana na maradhi ya Covid-19.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo wagonjwa wote walioripotiwa Tanzania bara wanaendelea kupata nafuu isipokuwa wanne ambao wanahitaji uangalizi maalum.
Kufikia sasa katika eneo la Tanzania bara wagonjwa wameambukizwa kama ifuatavyo kwenye mabano
Wagonjwa 23 kati hao 84 waliothibitishwa ni wale waliotolwa na Wizara ya Afya ya Zanzibar Jumatatu.