Home Uncategorized Mwili wa hayati rais JPM unaagwa Chato

Mwili wa hayati rais JPM unaagwa Chato

0 comment 89 views

Shughuli ya kutoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Rais wa Tanzania marehemu John Magufuli leo Alhamisi Machi 25, 2021 zinafanyika kwa wananchi wa wilaya ya Chato na maeneo jirani katika uwanja wa Magufuli uliopo kata ya Muungano na maziko yamepangwa kufanyika kesho Ijumaa wilayani humo.

Hadi leo kiongozi huyo ameagwa mkoani Dar es Salaam, jijini Dodoma, Mwanza na visiwani Zanzibar.

Rais Magufuli alifariki dunia Machi 17, 2021 katika hospitali ya Mzena mkoani Dar es Salaam kwa ugonjwa wa moyo.

Wananchi wameruhusiwa kuingia uwanjani mapema alfajiri huku vikosi vya ulinzi na usalama vikiimarisha ulinzi.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter