Home VIWANDAMIUNDOMBINU Daraja la Tanzanite kuanza kutumika February Mosi

Daraja la Tanzanite kuanza kutumika February Mosi

0 comment 225 views

Daraja la Tanzanite(Salenda) limekamilika kwa asilimia 100 na litaanza kutumika rasmi kesho February Mosi, 2022.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa amesema daraja hilo lenye urefu wa km 1.03 limegharimu kiasi cha Sh bilioni 243.

Amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha kuwa Tanzania inafunguka kwenye sekta ya miundombinu ili wananchi waweze kufanya kazi zao na nchi iweze kukua kiuchumi kwa asilimia 100.

“Daraja hili ni muhimu sana kwa sababu litapunguza changamoto ya foleni sababu daraja la zamani la Selanda lilikuwa limeshazidiwa na wingi wa magari hivyo kukamilika kwake ni muarobaini kwa foleni za jiji la Dar es Salaam”, amesema Prof. Mbarawa.

“Ufunguzi rasmi wa daraja hili tutaufanya hapo baadae, tutamualika Rais na yeye atafanya ufunguzi rasmi, lakini Jumanne tutawaruhu wananchi waweze kupita waweze kutumia daraja hili,” Prof.  Mbarawa.

Ameongeza kuwa daraja hilo litaruhusiwa kwa wananchi kulitumia bila malipo kwa saa 24 kwa siku.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter