Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Elisante Ole Gabriel ameagiza Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda nchini (Tirdo) kufanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha wadau wa biashara na viwanda wanapatiwa huduma muda wote.
Ole Gabriel ametoa agizo hilo baada ya kutembelea shirika hilo ambapo ameongeza kuwa ni lazima Tirdo ifanye kazi masaa 24 ili wafanyabiashara na wawekezaji wasikose huduma muhimu.
Katibu Mkuu huyo amedai kuwa mapinduzi ya viwanda ya viwanda huanza katika fikra za watu na sio katika mitambo na kusema shirika hilo hilo limekuwa msaada mkubwa kwa serikali katika kutambua maeneo yanayofaa zaidi kuanzisha viwanda.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Tirdo Prof. Mkumbukwa Mtambo amesema taasisi zinazofanya utafiti kuhusu maendeleo ya viwanda ni silaha kubwa ya ushindani kuelekea uchumi wa viwanda.