Home VIWANDAMIUNDOMBINU Kivuko kipya kujengwa Mwanza

Kivuko kipya kujengwa Mwanza

0 comment 116 views

Na Mwandishi wetu

Serikali imejipanga kujenga kivuko kipya mkoani Mwanza, kivuko ambacho kitafanya safari zake katika Ziwa Victoria kati ya Kigongo na Busisi. Ujenzi wa kivuko hicho ambao utagharimu kiasi cha Sh. 8.9 bilioni utafanya idadi ya vivuko katika eneo hilo kufikia vinne baada ya MV Sengerema, MV Sabasaba na MV Misungwi.

Akiwa katika uwekaji wa jiwe la msingi wa ujenzi huo, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dk. Mussa Ngwatu amesema kuwa wakazi wa Mwanza wanapaswa kujivunia mradi huu kwani pindi utakapokamilika, utasaidia kurahisisha usafiri wa wananchi na mali zao hivyo kuimarisha shughuli za kiuchumi.

Dk. Ngwatu mbali na hayo ameitaka Kampuni ya Songoro ya Mwanza ambayo imeshinda zabuni ya kujenga kivuko hicho kuhakikisha kuwa wanamaliza ujenzi katika muda uliopangwa huku wakizingatia ubora wa hali ya juu kama walivyokubaliana katika mkataba.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter