Home AJIRA JIAJIRI KUPITIA BIASHARA YA BAKERY

JIAJIRI KUPITIA BIASHARA YA BAKERY

0 comment 293 views

Katika harakati za hapa na pale ili kuwa na maisha bora na kipato cha uhakika, kujiajiri kumekuwa mkombozi wa watu wengi. Moja kati ya biashara ambazo hufanya vizuri sana hapa nchini ni utengenezaji wa keki. Biashara hii inaweza kuanzishwa kwa mtaji mdogo na kuendelezwa kadri siku zinavyoenda na biashara inavyokuwa. Ni biashara ambayo huweza kuendeshwa mwaka mzima kwani haiangalii msimu maalum. Yafuatayo ni baadhi ya mambo muhimu ya kuzingatia kama unafikiria kuanzisha biashara hii.

Umakini mkubwa unatakiwa wakati wa kutafuta eneo la biashara hii. Kama biashara nyingine, biashara hii inapaswa kuwa mahali ambapo watu wanaweza kuiona na kupata huduma kwa urahisi. Angalia eneo ambalo lina mzunguko mkubwa wa watu kwani inakuwa fursa nzuri kujitangaza na kuwafikia wateja wengi kwa wakati mmoja.

Ni muhimu kuwa na vifaa vyote vinavyohitajika kutengeneza bidhaa bora. Biashara ya kutengeneza keki haiwezi kufika mbali bila ya kuwa na vifaa hivyo kabla ya kufungua biashara hii ni vizuri kuwa na uhakika wa vifaa ili kuepuka usumbufu wa aina yoyote baada ya kufungua biashara yako. Vilevile kutokana na biashara hii kutegemea umeme kwa asilimia 100 ni muhimu kuwa na jenereta ili kutopata hasara kila tatizo la umeme linapojitokeza.

Hakikisha umefuata taratibu zote zilizowekwa na mamlaka husika ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza. Ni muhimu kusajili jina la biashara yako, kupata leseni, kupata TIN, kuwa na kibali kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na taratibu nyingine ili kuhalalisha ubora wa bidhaa zako na vilevile kuwapa wateja uhakika kuwa kile unachofanya kinatambulika na mamlaka husika.

ADVERTISEMENT

Kama ilivyo kwa biashara nyingine yoyote ni lazima kuwa mbunifu katika utengenezaji wako wa keki. Usiogope kuwa tofauti na kufanya vitu ambavyo watu wengi hawafanyi. Ubunifu ni muhimu sana katika biashara hii kwani ndio kitu pekee ambacho kitafanya bidhaa yako kupendwa na kupokelewa vizuri sokoni. Hivyo usichoke kujifunza kutoka kwa wengine, kusikiliza ushauri na hata kutumia mitandao tofauti kufahamu zaidi ili uwapatie wateja wako kilicho bora.

Biashara hii imeweza kuonyesha mafanikio kwa wengi ambao wanaifanya. Ni muhimu kuwa na malengo na kufanya kazi kwa bidii ili kuyatimiza. Pia biashara hii ni moja kati ya biashara ambayo inaweza kuendeshwa na familia au kundi la wajasiriamali au mtu mmoja kama wengine wanavyofanya. Kwa wale wanaofikiria kujiajiri, biashara hii ni fursa nzuri endapo una ujuzi na utaalamu wa kutosha. Vilevile, unaweza kusomea na kujifunza kutengeneza keki kisha kujiajiri mwenyewe na kujiingizia kipato,.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter