Home BENKI Wafanyabiashara washauriwa kuchangamkia kituo

Wafanyabiashara washauriwa kuchangamkia kituo

0 comment 103 views

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dk. Stephen Kebwe ametoa wito kwa wafanyabiashara mkoani humo kutumia vizuri uwepo wa kituo cha biashara cha benki ya NMB ili kuwa katika nafasi nzuri ya kupata fursa za mitaji na masoko. Dk. Kebwe amesema hayo wakati wa uzinduzi wa kituo hicho cha NMB akisisitiza kuwa, kituo hicho kinalenga kuwasaidia wafanyabiashara kutoka mkoani humo.

Katika hotuba yake imeelezwa kuwa NMB imewekeza katika kituo hicho kutokana na fursa lukuki za kiuchumi zilizopo mkoani Morogoro kama vile kilimo, utalii pamoja na madini huku wakazi wa mkoa huo wakishindwa kufaidika na rasilimali zinazowazunguka. Kituo hicho mbali na kuwaunganisha wafanyabiashara na kuwapatia elimu pia kitatoa huduma ya utoaji mikopo.

Akizungumzia uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa NMB Ineke Bussemaker amesema kituo hicho cha Morogoro ni kituo cha kumi hapa nchini akifafanua kuwa lengo la kuanzisha vituo hivyo ni kusaidia wafanyabiashara na shughuli zao.

“Tumekuwa tukiunga mkono serikali katika jitihada zake mbalimbali ikiwemo kusaidia kukusanya kodi na sasa katika kuelekea uchumi wa viwanda tumeelekeza juhudi zetu kuwasaidia wafanyabiashara kwa kuanzisha kituo maalum ambacho watakutana na maofisa wetu na kuwapatia ushauri”. Ameeleza Bussemaker.

Mbali na kuzindua kituo hicho, benki ya NMB pia imetoa msaada wa madawati yenye thamani ya Sh. 10 milioni kwa shule za sekondari Lupanga na Kilakala zilizopo katika manispaa ya Morogoro.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter