Home BIASHARABIASHARA NDOGO NDOGO Ugawaji vitambulisho umalizike Machi-Makonda

Ugawaji vitambulisho umalizike Machi-Makonda

0 comment 126 views

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amewataka wakuu wa wilaya zote kuhakikisha kuwa hadi kufikia 01/03/2019, kila mfanyabiashara ndogondogo anakuwa na kitambulisho rasmi kilichotolewa na Rais Magufuli. Makonda amesema hayo alipokutana na viongozi mbalimbali jijini Dar es salaam na kutoa wito kwa wafanyabiashara kuchangamkia fursa hiyo.

Makonda ameeleza kuwa baada ya tarehe moja mwezi Machi, mfanyabiashara yeyote atakayekutwa bila kitambulisho, leseni ya manispaa au vielelezo vya kulipa kodi kutoka TRA atachukuliwa hatua kwa mujibu wa Sheria.

Aidha, Mkuu huyo wa mkoa amegawa vitambulisho vya wafanyabiashara ndogondogo kwa wakuu wa wilaya na hivyo kufanya mkoa huo kuwa kinara kwa kupokea takribani vitambulisho 175,000 kutoka kwa Rais. Na kutoa onyo kwa watendaji wanaowatoza wafanyabiashara kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya vitambulisho tofauti na bei elekezi ya Sh. 20,000.

Pamoja na kutoa vitambulisho, Makonda ametoa miezi miwili kwa Wakurugenzi wa Manispaa kuhakikisha leseni za wafanyabiashara zinaingizwa katika mfumo mmoja ikiwa ni pamoja na kuharakisha utoaji wa leseni ili kupunguza kero kwa wananchi.

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter