Home BIASHARA Kampeni ya Tuzo Points yanoga

Kampeni ya Tuzo Points yanoga

0 comment 38 views

Kampuni ya mawasiliano kupitia simu za mkononi, Vodacom Tanzania imewatembelea wakazi wa Mbagala jijini Dar es Salaam na kutoa elimu ya kampeni ya tuzo points ‘ Baki Mule Mule Utunzwe na Tuzo Points’.

Vodacom Tanzania pia inawazawadia wateja wao Point za Tuzo zenye thamani ya shilling Bilioni moja katika msimu huu wa sikukuu.

Mtoa huduma wa Vodacom Tanzania, Bi. Stella Richard akizungumza na kumuelimisha mfanyabiashara jinsi ya kuzipata na kuzitumia pointi za Tuzo, hapo jana katika kampeni ya Tuzo points ‘Baki Mule Mule Utunzwe na Tuzo Points’ iliyofanyika eneo la Mbagala Charambe na Chamazi jijini Dar es Salaam. Katika msimu huu wa sikukuu Vodacom Tanzania inawazawadia wateja wao Point za Tuzo zenye thamani ya shilling Bilioni moja.

Kiongozi wa Timu ya watoa huduma wa Vodacom Tanzania, Nashon Leonard akizungumza na watoa huduma wa Vodacom Tanzania mara baada ya kumaliza kutoa elimu ya kampeni ya Tuzo Points ‘Baki Mule Mule utunzwe na Tuzo Points’ iliyofanyika eneo la Mbagala Charambe na Chamazi jijini Dar es Salaam.

Kikundi cha burudani kinachofahamika kwa jina la Respect Crew wakitoa burudani kwa wakazi wa Mbagala wakati wa utoaji elimu wa kampeni ya Tuzo Points ‘Baki Mule Mule utunzwe na Tuzo Points’ jijini Dar es Salaam.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter