Home BIASHARA Wanaokwepa kodi ya madini kubanwa

Wanaokwepa kodi ya madini kubanwa

0 comment 82 views

Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo amesema serikali haitamvumilia mchimbaji yoyote wa madini atakayekimbia kulipa kodi kwani ni kinyume na Sheria ya Madini na kanuni zake. Nyongo amesema hayo wakati wa mkutano wake na wachimbaji wadogo wa madini katika machimbo ya Reef D mkoani Katavi, ikiwa ni sehemu ya ziara yake katika mkoa huo.

Katika ziara hiyo, Naibu Waziri huyo ameambatana na Mkuu wa wilaya ya Tanganyika,  Salehe Mhando, Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji wa Madini Mkoa wa Katavi (KATAREMA), William Mbongo, Kaimu Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Katavi, Mhandisi Giliard Luyoka, wataalamu wa madini, vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na waandishi wa habari.

Nyongo ameeleza kuwa kumekuwa na tabia ya baadhi ya wachimbaji kukwepa kulipa kodi hali inayopeleka kukosekana kwa upatikanaji wa huduma nyingine za msingi katika jamii kama vile elimu, maji na miundombinu ya barabara.

“Mchimbaji ambaye anakwepa kulipa kodi mbalimbali kama Sheria ya Madini na kanuni zake inavyofafanua ni adui namba moja katika ukuaji wa maendeleo ya nchi, hivyo sisi kama Wizara ya Madini tumejipanga kuchukua hatua za kisheria nia ikiwa ni kutaka kila mwananchi anufaike na rasilimali za madini kupitia uboreshaji wa huduma mbalimbali”. Amesema Nyongo.

Naibu Waziri Nyongo pia amewataka maafisa madini wakazi katika mikoa yote kuwa wabunifu katika ukusanyaji wa maduhuli huku akisistiza kuwa, sekta ya madini inachukua nafasi kubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter