Home Elimu Vijana wanasajili bunifu nchi jirani: Nape

Vijana wanasajili bunifu nchi jirani: Nape

0 comment 192 views

Kukosekana kwa Sera ya kampuni changa (Startups) kunawafanya baadhi ya vijana wa Tanzania kusajili bunifu zao nchi jirani.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye amesema hayo katika kikao cha wadau mbalimabli kutoka ndani na nje ya nchi cha kujadili ushirikiano wa maendeleo juu ya uundwaji wa Sera ya Kampuni Changa za TEHAMA (Startups) Tanzania kilichofanyika mwishoni mwa mwezi Oktoba jijini Dar es Salaam.

Waziri Nape amesema kuwa baadhi ya vijana wabunifu wa TEHAMA imewabidi wakasajili bunifu zao katika nchi za jirani kutokana na kutokuwepo kwa Sera ya Startups nchini.

“Bahati mbaya kwa muda kidogo nchi yetu imekuwa haina mfumo mzuri wa kisheria wa vijana hawa wanaofanya ubunifu katika TEHAMA na mara nyingi wamelazimika kwenda nje ya nchi ili kusajili bunifu zao.

Kama Serikali tukasema inabidi tuwe na mfumo mzuri utakaotambua bunifu za hawa vijana lakini pia uweze kuzilinda bunifu hizo ili pia waweze kuvutia uwekezaji nchini,” amesema Waziri Nape.

Amebainisha kuwa serikali imekubaliana na wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi, kuweka misingi na wako tayari kuendelea na hatua inayofuata ili kukamilisha sera hiyo mapema.

Kikao hicho pia kimewahusisha Wadau mbalimbali wakiwemo Wadau wa Maendeleo nchini, Chama cha Tanzania Startups Association, Taasisi za Serikali na Wizara mbalimbali.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter