Home FEDHAMIKOPO Urejeshaji mikopo bado changamoto

Urejeshaji mikopo bado changamoto

0 comment 30 views

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Joachim Wangabo ametoa wito kwa wananchi wa mkoa huo kuwa na nidhamu ya fedha na kujenga mazoea ya kurejesha mikopo kwani mikopo wanayopatiwa haitowasaidia kama inatumika tofauti na malengo yaliyokusudiwa. Wangabo ametoa ushauri huo wakati akikabidhi mkopo wa Sh. 70 milioni uliotolewa na Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga maalum kwa ajili ya vikundi 25 vya wanawake, walemavu na vijana.

 

Katika maelezo yake, Wangabo amesema changamoto kubwa katika mkoa huo ni wananchi kutokuwa na utamaduni wa kurejesha mikopo kwa sababu walio wengi wamekuwa wakitumia fedha hizo tofauti na malengo. Mkuu huyo wa mkoa amesema Halmashauri zimekuwa zikitenga asilimia 10 ya makusanyo ya ndani kwa ajili ya mikopo lakini idadi kubwa ya vikundi vilivyonufaika na mikopo hiyo vimeshindwa kufanya marejesho.

 

Naye Meya wa Manispaa ya Sumbawanga, Justin Malisawa amesema mwaka jana, Halmashauri hiyo ilikopesha takribani Sh. 40 milioni kwa vikundi lakini hadi kufikia sasa, ni Sh. 16 milioni pekee zilizorejeshwa, hali ambayo amedai inapelekea vikundi vingine kukosa fursa ya kupata mikopo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter