• Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI
Sunday, January 29, 2023
  • Login
  • Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI
No Result
View All Result
Pesatu
  • Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI
No Result
View All Result
Pesatu
No Result
View All Result

Waziri Mkuu: Serikali yawapa wakulima mikopo ya Sh. 56.45 bilioni

Patricia Richard by Patricia Richard
October 4, 2018
in MIKOPO
0
Majaliwa ataka benki kushusha riba

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa.

Share on FacebookShare on Twitter

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema serikali imetoa mikopo yenye thamani ya Sh. bilioni 56.45 kwa ajili ya miradi mbalimbali ya kilimo katika mikoa 13 hapa nchini. Amesema mikopo hiyo imetolewa katika kipindi cha kuanzia Agosti 2015 hadi Septemba 2018, kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB).

Waziri Mkuu ameyasema hayo jana (Jumatano, Oktoba 3, 2018) kwenye maadhimisho ya miaka 25 ya Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA) mjini Morogoro. Mikopo hiyo imewanufaisha wakulima wadogo zaidi ya 527,000 waliopo kwenye mnyororo wa thamani wa mazao ya kahawa, karafuu, mahindi, mbogamboga na mazao mengine.

Amesema serikali inatekeleza mipango mbalimbali kwa lengo la kutatua kero zinazowakabili na kuwawezesha wakulima wadogo kujikwamua kiuchumi kupitia kilimo.  Amesema Juni 14, mwaka huu Rais Dkt. John Magufuli, alizindua Awamu ya Pili ya Programu ya Kuendeleza Kilimo hapa nchini (ASDP II) yenye lengo la kuboresha sekta ya kilimo.

Waziri Mkuu amesema ASDP II inalenga kuhakikisha sekta ya kilimo inapewa kipaumbele stahiki ili iweze kuleta tija kwa wakulima wenyewe na taifa kwa ujumla.

“Serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuboresha sekta ya kilimo ikiwemo kutoa mikopo kwa wakulima wadogo; kuondoa baadhi ya tozo zenye kufifisha uzalishaji.”

ADVERTISEMENT

Pia kuweka mipango mizuri ya matumizi bora ya ardhi na kutafuta masoko pamoja na kuongeza thamani kwenye mazao ya kilimo ili kumuongezea tija mkulima. Kadhalika, Waziri Mkuu ameongeza kuwa mchango wa wakulima wadogo umewezesha taifa kujitosheleza kwa chakula na hata kuuza nje ya nchi mazao ya kilimo.

Hivyo, Waziri Mkuu ametoa rai kwa viongozi na watendaji wa serikali kujenga utamaduni wa kuhudhuria wa kukutana na kuzungumza na wakulima kuhusu mahitaji hayo.

“Tunafahamu kwamba wakulima mna changamoto nyingi zikiwemo za kisera, kirasilimali na kiutendaji kwenye masuala ya ardhi, masoko, mitaji na hata kero za tozo na ushuru.”

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameagiza Wakala wa Vipimo nchini (WMA) waendesha msako utakaowanasa wafanyabiashara wanaowaibia wakulima  kwa  njia ya udanganyifu wa kutumia vipimo visivyo sahihi. Waziri Mkuu amesema mfanyabiashara yeyote atakayebainika kuwaibia wakulima  kwa kutumia vipimo visivyo rasmi achukuliwe hatua za kisheria.

“Utaratibu wa kutumia vipimo visivyo rasmi ambavyo vimepewa majina ya lumbesa, kangomba, umejileta mwenyewe na mengine mengi lazima ukomeshwe.”

Waziri Mkuu  ameuagiza uongozi wa WMA kwa kushirikiana na halmashauri zote nchini wahakikishe mazao ya wakulima yanauzwa kwa kutumia vipimo rasmi ili wasiendelee kupunjwa. Akizungumzia kuhusu kero ya ardhi, Waziri Mkuu amesema  Serikali itawapa wananchi  ardhi inayotwaliwa kutoka kwa  wawekezaji au wamiliki walioshidwa kukidhi masharti  na yale yasiyoendelezwa kwa muda mrefu.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Tags: ASDP IIKassim MajaliwakilimomikopoMviwataTADBWMA
Patricia Richard

Patricia Richard

Next Post
Kaimu Mkurugenzi  Mkuu wa Vodacom Tanzania PLC, Hisham Hendi (kulia) akimhudumia mteja Rafi Soule, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya huduma kwa Mteja katika duka la Vodacom lililopo makao makuu ya kampuni hiyo  Morocco jijini Dar es salaam.Katikati ni Mkurugenzi wa  Huduma kwa wateja (Customer Care) Harriet Lwakatare.

Vodacom yasherehekea Wiki ya Wateja

Discussion about this post

Habari Mpya

Poland kuisaidia Tanzania kuweka mifumo ya kodi kidigitali

January 26, 2023

Kamati ya bunge yahimiza uwekezaji maeneo ya hifadhi

January 21, 2023

Serikali kuanzisha mnada wa chai

January 20, 2023

Tumieni bandari ya Dar es Salaam: Makalla

January 19, 2023
Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza katika Jukwaa la Uchumi Duniani.

Sekta ya kilimo kukua kwa 10% 2030: Rais Samia

January 19, 2023

Ndege tano kuwasili mwaka huu

January 17, 2023

KUHUSU SISI

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905. PesaTu inamlenga kila mtu ambaye kwa namna moja au nyingine anaguswa na anapenda kujua/ kufuatilia masuala mbalimbali ya kiuchumi ya nchi ikiwemo ujasiriamali, uwekezaji, viwanda, kilimo na hisa.

LATEST

Poland kuisaidia Tanzania kuweka mifumo ya kodi kidigitali

by Pesatu Reporter
January 26, 2023
0

Poland imeahidi kuisadia Tanzania kuimarisha mifumo ya kodi kwa njia ya kidigitali ili kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato ya...

Kamati ya bunge yahimiza uwekezaji maeneo ya hifadhi

by Pesatu Reporter
January 21, 2023
0

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeishauri Wizara ya Maliasili na Utalii iendelee kuzifanyia maboresho kanuni...

RECOMMENDED

Waziri Mwijange aja na orodha ya viwanda visivyofanya kazi

by Patricia Richard
March 23, 2018
0

  Na Mwandishi wetu. Baada ya Rais John Magufuli kuonyesha kukerwa na kitendo cha Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji...

Nane Nane itumike kama darasa huru kwa wakulima

by Patricia Richard
March 23, 2018
0

Na Mwandishi wetu Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imejitolea kuwapa mafunzo ya siku moja wakulima mkoani Lindi...

No Result
View All Result
  • Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI

© 2023 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In