Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKIUJASIRIAMALI Ubunifu wa Furniture ni fursa tosha

Ubunifu wa Furniture ni fursa tosha

0 comment 50 views

Kutokana na changamoto ya ajira nchini, vijana wengi wameamua kujiongeza na kuwa wabunifu. Ubunifu huu si tu kwa wasomi pekee, bali hata walioishia darasa la saba wamekua wakiufanya au kuiga wakiendeleza pale walipoishia wengine.

Moja ya faida ya kukosekana kwa ajira ni kukua kwa ubunifu hasa wa kibiashara na hivyo kupelekea kukua kwa biashara ya furniture za majumbani na hata maofisini. Biashara hii ilikua ikifanywa kwa uchache na mafundi seremala ambao walijikita zaidi katika kutengeneza vitu kama madirisha na milango huku furniture za ndani hasa sebuleni wakizipa umuhimu kiduchu.

Ushindani ni kitu kizuri na kinalipa, baada ya kuwapo kwa wimbi kubwa la vijana waliokimbilia ufundi stadi hasa useremala na hivyo kuongeza idadi ya mafundi mtaani na ushindani kukua, hali ambayo kwa kiasi kikubwa imepelekea ubunifu kuongezeka na jamii kuanza kupata matokeo chanya.

Kupendeza kwa mandhari ya sebule na varanda za nyumba mbalimbali nchini ni matokeo ya ubunifu huu wa mafundi seremala. Vijana wengi wamejikita katika kutengeneza meza za kuwekea televisheni na maua, meza zakahawa (coffee table), meza za chakula (dining table), seti za masofa,vitanda vya wakubwa na watoto, makabati ya nguo na vyombo n k.

Biashara hii licha ya kutatua changamoto ya ajira, pia imeongeza kipato cha mtu na mtu, familia na taifa kwa ujumla.Ubunifu katika furniture umepelekea kuongezeka kwa soko la wanaozitumia hivyo baadhi ya vijana wameamua kuanzisha viwanda vidogo ambavyo vinaliingizia taifa kodi ya mapato.

Licha ya kukua na kupendwa kwa furniture hizi za mitaani, baadhi ya mafundi wamekuwa sio waaminifu kwa kuchukua pesa za wateja na kutokomea kusikojulikana ama kutokabidhi kazi kwa wakati kama inavyopaswa. Vijana wanatakiwa kuwa waaminifu kwa wateja, pia warasimishe biashara zao kwa kujenga jina na kuwa na eneo maalumu la kufanyia kazi(work shop) ili kuongeza uaminifu na ufanisi.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter