Home KILIMOKILIMO BIASHARA Baadhi ya mazao yaliyopanda bei mwaka 2024

Baadhi ya mazao yaliyopanda bei mwaka 2024

0 comment 42 views

Mwaka 2024 umekuwa wa neema kwa wakulima kwa baadhi ya mazao kupanda bei ikilinganishwa na mwaka 2023.

Mazao hayo ni pamoja na ufuta, korosho, kakao, kahawa na mbaazi.

Akitoa salamu za mwaka mpya 2025, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alisema serikali kupitia Sekta ya Kilimo imeongeza uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara pamoja na kuboresha mfumo wa masoko ya kilimo ambapo imepelekea kupanda kwa bei ya mazao kwa mwaka 2024.

Rais Samia ameeleza kuwa, kwa mwaka 2024 ufuta uliuzwa kwa Tsh 4,850 kwa kilo ikilinganishwa na Tsh 3,600 mwaka 2023.

“Kahawa aina ya Arabika iliuzwa kwa shilingi 8,500 kwa kilo ikilinganishwa na shilingi 6,500 kwa mwaka uliopita, na kwa kahawa aina ya Robusta iliuzwa kwa Tsh 5,000 kwa kilo badala ya shilingi 3,500 ya mwaka 2023,” amaeeleza Rais Dkt. Samia.

Kwa upande wa mbaazi Rais Dkt. Samia amesema iliuzwa kwa Tsh 2,236 kwa kilo mwaka 2024 badala ya Tsh 2,000 mwaka 2023.

Kakao imeuzwa kwa Tsh 35,000 kwa kilo ikilinganishwa na bei ya Tsh 29,500 kwa mwaka 2023.

Rais Samia amebainisha kuwa korosho iliuzwa kwa Tsh 4,165 kwa kilo ikilinganishwa na Tsh 2,190 kwa mwaka 2023.

“Uzalishaji wa korosho unatarajiwa kufikia tani laki na ishirini na tano, mia mbili na tano kwa msimu huu tulio nao wa mwaka 2024/2025 unaoendelea ukilinganishwa na tani laki tatu na elfu kumi, mia saba themanini na saba zilizozalishwa msimu uliopita wa 2023/2024.

Mwelekeo wa serikali ni kuboresha stakabadhi za ghala kupitia soko la bidhaa Tanzania (TMX) kwa mazao ya kilimo,” amasema Rais Dkt. Samia.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter