Home VIWANDAMIUNDOMBINU Waziri Mbarawa atoa neno TAA

Waziri Mbarawa atoa neno TAA

0 comment 63 views

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, amesema suala la usalama katika viwanja vya ndege linapaswa kupewa kipaumbele ili kuepuka majanga kama lile la Mwanza ambapo mtu mmoja alipoteza maisha kwa kugongwa na ndege. Prof. Mbarawa amesema hayo katika uzinduzi wa baraza jipya la wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) jijini Dar es salaam.

Mbali na hayo, Waziri huyo amewataka wanafanyakazi wa TAA kuongeza juhudi ili kufikia lengo waliojiwekea la kukusanya Sh.134 bilioni kwa mwaka mpya wa fedha unaoanza Julai mosi mwaka huu. Ameongeza kuwa lengo hilo likifanikiwa na mapato yakijitosheleza, mamlaka hiyo inaweza kujipanga na kuwaongezea watumishi wake mishahara

Prof. Mbarawa pia ameshauri TAA kutotegemea mapato yatokanayo na viwanja moja kwa moja pekee na badala yake, watumie fursa mbalimbali zilizopo kutengeneza faida zaidi. Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo Richard Mayongela amesema kuwa jitihada za kuboresha ulinzi na usalama katika viwanja mbalimbali vya ndege nchini tayari zimeshaanza na ujenzi wa uzio katika uwanja wa ndege wa Mwanza unaendelea.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter