Home FEDHAHISA Tofauti ya soko la hisa na soko la dhamana

Tofauti ya soko la hisa na soko la dhamana

0 comment 276 views

Kwenye uwekezaji kuna pande mbili, upande wa pmiliki na upande wa ukopeshaji. Kwa kifupi, ukiongelea soko la hisa unaongelea upande wa umiliki na ukiongelea soko la dhamana unaongelea ukopeshaji.

Hivyo basi tuaangalia maana ya masoko haya mawili na tofauti iliyopo kati yao ili muwekezaji aweze kufanya maamuzi sahihi.

Soko la hisa ni nini?

Hisa peke yake ni kipande cha umiliki ambacho huuzwa na kampuni ambapo mnunuzi wa kipande hicho huwa mmiliki wa kampuni hiyo kutokana na asilimia za hisa alizonunua. Hisa ni mahali pa biashara za hisa za makampuni.

Soko la hisa likipanda, wamiliki hupata faida na pale soko linaposhuka wamiliki hupata hasara. Uwekezaji huu hufanywa na watu binafsi au makampuni kwenye makampuni mengine. Kwa Tanzania, makampuni huuaza hisa zao kwa wanunuzi kupitia taasisi inayofahamika kama Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE).

Soko la dhamana/Mtaji ni nini?

Soko hili haliongelewi sana lakini ni moja ya masoko ambayo mtu akiwekeza anakuwa na uhakika wa kupata fedha. Ni soko ambalo linahusisha ukopaji ambapo mtu aliyekopeshwa kusaini mkataba wa kulipa riba asilimia fulani kwa kipindi fulani na mwisho wa  malipo mkopaji hutakiwa kulipa kiasi taslimu alichokopeshwa. Kwa mfano A amemkopesha bilioni kadhaa B kwa makubaliano ya kulipa asilimia X kila mwaka kwa kipindi cha miaka 5 na baada ya miaka hiyo mitano atarudisha zile fedha za mwanzo kabisa alizokopeshwa.Mkopeshaji hupata faida kutoka kwenye riba na fedha za mwanzo ambazo ni mtaji aliompa mkopaji.

Inaelezwa kuwa, Marekani inafanya uwekezaji huu kwa asilimia 44. Mara nyingi soko la dhamana hufanywa na taasisi binafsi, serikali na hata watu binafsi.

Tofauti:

  • Soko la hisa lina hatari kubwa kuliko soko la dhamana/mtaji kwa sababu, kama soko hilo litashuka na kupelekea kampuni kufungwa basi wamiliki wote wa hisa hawatapata chochote. Kwenye soko la dhamana/mtaji, mkopeshaji anakuwa na uhakika wa riba na hata kama mkopaji akifilisika kabisa baada ya muda wa kulipa deni lake mkopeshaji atakuwa amepata kiasi kadhaa cha fedha zake hata kama hatopata mtaji wake hivyo ataondokana na hasara.

Mfano (Hisa): Asilimia 50 ya hisa za kampuni ni Sh. 5 milioni. Hisa  zimeongezeka thamani 50% au 40% au hata 5% mmiliki wa 50% atanufaika kutokana na ongezeko hilo. Endapo hisa hizo zitapungua asilimia 50%, basi mmiliki hatopata chochote.

Mfano (Dhamana/Mtaji): Mkopeshaji akimkopesha mtu Sh. 5 milioni na wakakubaliana awe analipa asilimia 4% kila mwaka basi mkopeshaji atapata riba ya asilimia 4 kila mwaka na mwisho wake mkopaji atalipa pia fedha alizopewa mwanzo. Hata kama mkopaji akifika kati na kushindwa kuendelea kulipa, mkopeshaji atakuwa amepata kiasi kadhaa kutokana na riba.

Kwa ujumla, uwekezaji katika hisa ni hatari zaidi kuliko uwekezaji katika soko la dhamana ila kitendo cha hisa kupanda kinaweza kukuingizia fedha nyingi. Ni muhimu kufanya maamuzi sahihi kuhusu aina hii ya uwekezaji.

 

 

 

 

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter