Kama ilivyo kwa biashara nyingine kupanda na kushuka kwa bei, ndivyo ilivyo katika biashara ya makopo ya plastiki na chupa za maji.
Kwa sasa bei ya makopo na chupa za plastiki imeshuka kutoka Sh. 500 kwa kilo moja hadi kufikia Sh. 350 kwa kilo.
“Kwa sasa bei imeshuka na itaendelea kushuka, leo tuinanunua kwa Sh. 450 lakini kesho huenda ikafika 350, hii ni kawaida kwa msimu huu wa mwishoni mwa mwaka kutokana na wanunuzi wakuu ambao ni Wachina wanasafiri kwenda China,” anasema mnunuzi wa makopo eneo la Kimara.
Anaeleza kuwa kuanzia mwezi Oktoba bei huanza kushuka hadi kufikia mwezi Disemba ambapo wanunuzi huwa katika kipindi cha sikukuu za mwisho wa mwaka.
Soma zaidi: