Home BIASHARA Dar yajipanga Biashara masaa 24

Dar yajipanga Biashara masaa 24

0 comment 128 views

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amethibitisha kuwepo kwa mchakato ili kuruhusu kufanyika kwa biashara masaa 24 ndani ya jiji la dar es salaam ili kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi na mapato kwa serikali.

Akizungumza na waandishi ofisini kwake ilala jijini dar es salaam amesema ofisi yake ipo katika mchakato wa kukutana na wafanyabiashara ili kujadili jinsi ya kufanikisha suala hilo hasa kuhakikisha suala la usalama wa biashara na raia.

“Kabla hatujawaruhusu wafanyabiashara kufanya kazi masaa 24 lazima tujiandae na kuhakikisha wamiliki nao wanajiandaa pia tufunge taa za usalama na kamera kuzuia uhalifu”,alisema makonda

Ikumbukwe hapo nyuma serikali ilizuia ufanyaji wa biashara chini ya saa kumi jioni na zaidi ya saa 6 usiku kwa biashara za pombe (baa) hali iliyopelekea kushuka kwa mzunguko wa biashara hiyo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter