Home BIASHARABIASHARA NDOGO NDOGO Machinga kuhamishwa Ubungo

Machinga kuhamishwa Ubungo

0 comment 140 views

Waziri Mkuu ameagiza wafanyabiashara wadogo wanaofahamika zaidi kama machinga kuondolewa eneo la Ubungo, Dar es Salaam ili kupisha ujenzi wa barabara za juu unaoendelea katika eneo hilo. Majaliwa ametoa agizo hilo alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara hizo na ujenzi wa daraja la juu eneo la Tazara ambapo amesema kuondolewa kwa wafanyabiashara hao kutampa nafasi mkandarasi kutekeleza majukumu yake bila kikwazo na hivyo kukamilisha mradi kwa wakati.

Waziri Majaliwa amewataka Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe pamoja na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuhakikisha wafanyabiashara hao wanaondolewa na kupelekwa katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili yao.

Ujenzi wa daraja hilo kwenye makutano ya barabara za Morogoro, Mandela na Sam Nujoma eneo la Ubungo, unatekelezwa na kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC).

Akizungumzia kuhusu mradi huo, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Patrick Mfugale amedai ujenzi wa barabara hizo za juu, utakamilika ndani ya miezi 30. Kwa maelezo ya Tanroads, mradi huo unatekelezwa kwa mkopo wa Dola za Marekani 450 milioni kutoka Benki ya Dunia.

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter