Home BIASHARA JE UNA KADI ZA BIASHARA?,SOMA KUJUA UMUHIMU WAKE

JE UNA KADI ZA BIASHARA?,SOMA KUJUA UMUHIMU WAKE

0 comment 72 views

Kadi zimekuwa muhimu sana kwa wafanyabiashara hususani katika suala zima la kukuza mtandao wa biashara zao. Kadri muda unavyokwenda na uboreshwaji wa teknolojia za mawasiliano kadi za biashara zimeonekana kupoteza umuhimu wake kwa kiasi kikubwa na kuwafanya wafanyabiashara wengi kutokuwa nazo.

Ikiwa wewe ni mfanyabiashara unatakiwa kutambua kuwa kadi ni muhimu wakati wowote kwa sababu zifuatazo:

Teknolojia zimerahisishwa kwa kiasi kikubwa na hivi sasa inawezekana kusambaza habari mbalimbali kutoka katika simu moja kwenda nyingine ili mradi watumiaji wote wawe wanatumia simu za aina moja. Hivyo hata kama unaweza kubadilishana habari zako za mawasiliano na mteja ambaye anatumia simu kama chako haimaanishi itawezekana kwa kila mteja. Ili kurahisisha mawasiliano, tengeneza kadi za biashara na kumpatia kila mteja ambaye utawasiliana naye.

Sio kila mtu anatumia smartphone na mwenye uelewa wa kupata mawasiliano katika mitandao ya kijamii. Ili kurahisisha utoaji wa mawasiliano kwa wateja ni vyema kuwafikiria wale wasiotumia mtandao. Hii itawavutia kununua bidhaa kila watakapoihitaji kupitia mawasiliano yaliyopo katika kadi ya biashara yako.

Kadi zinaweza kutumika hata katika maeneo ambayo hakuna mtandao kama kijijini au sehemu ambazo hairuhusiwi kutumia simu kama vile kwenye ndege au hospitalini. Kwa kutoa kadi ya biashara unawapa wateja uhakika wa kukupata kirahisi.

Kadi ya biashara huongeza uhalali kwenye biashara. Siku zote watu hupendelea zaidi kujihusisha na biashara ambazo zinaaminika. Kuwa na kadi kutawaaminisha wateja kuhusu huduma zako na umakini ulionao hivyo kununua bidhaa zako kwa uhuru zaidi.

Kwa kugawa kadi za biashara ni dhahiri kuwa unakuza biashara yako kwani mteja husika baada ya kufurahishwa na huduma au bidhaa zako atatumia mawasiliano uliyompa kwa watu wengine ili nao waweze kujipatia bidhaa au huduma. Ni muhimu kuweka habari zote muhimu kuhusu biashara yako katika kadi yako ya biashara.

Mitandao imeendelea kuleta mafanikio makubwa lakini wafanyabiashara bado wana nafasi kubwa ya kukuza mitandao yao kwa kubadilishana kadi ili kuweza kupeana fursa mpya za kibiashara na uwekezaji, kubadilishana ujuzi na uzoefu na kuongeza mauzo katika biashara.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter