Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) Godfrey Simbeye amesema biashara nyingi zinafungwa kutokana na uwepo wa mazingira magumu pamoja na sera ambazo kwa kiasi kikubwa zinawakandamiza wafanyabiashara. Simbeye ametoa kauli hiyo mkoani Morogoro katika kongamano la kambi ya ujasiriamali lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Mzumbe.
Simbeye ameeleza kuwa kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na TPSF, takribani biashara 4,640 zimefungwa ndani ya miaka mitatu kutokana na vikwazo mbalimbali. Ameongeza kuwa TPSF imejipanga kusaidia sekta ya ujasiriamali pamoja na kutoa elimu.
Mbali na hayo, Simbeye ameshauri wanafunzi kuandaliwa na kufundishwa zaidi kuhusu ujasiriamali mapema na kusema kuwa ajira nyingi zaidi zinatokana na sekta hiyo. Amewataka vijana kujiamini na kuondokana na uwoga kwani wao ndio waathirika wakubwa wa tatizo hili.
Discussion about this post