Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKI Maliasili na Utalii kutumia akili bandia (AI)

Maliasili na Utalii kutumia akili bandia (AI)

0 comment 138 views

Wizara ya Maliasili na utalii imesema inaanza kutumi akili bandia (Artificial Intelligence) katika kutekeleza majukumu yake ili kuleta ufanisi wenye tija katika tafiti za Wanyama.

Imeeleza kuwa hivi karibuni itaanza kutumia AI kwenye kuandikisha watalii kutokea nchi wanazotoka hadi kwenye vivutio vya utalii watakavyotembelea.

Haya yamebainika wakati Kamati ya Bunge ya kudumu ya Ardhi, Maliasili na Utalii ikipokea taarifa ya utekelezaji wa taasisi zilizochini ya wizara ya maliasili na utalii ambazo ni Mradi wa uendelezaji utalii Kusini (REGROW), Chuo cha usimamizi wa wanyamapori Mweka (CAWMM) na Taasisi ya taaluma ya wanyamapori Pasiansi(PWTI).

Taasisi ya utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI) hutumia akili bandia katika kufanya sensa ya Wanyama waliopo kwenye hifadhi na mapori ya akiba.

Matumizi hayo ya akili bandia yameleta matokeo chanya hasa katika kupunguza gharama na muda wakati wa kufanya zoezi hilo.

Katika kikao hicho ambacho kilihudhuriwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Danstan Kitandula(MB),

Akijibu hoja za kamati, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Hassan Abbasi amesema Wizara imekuwa ikiweka msisitizo wa kufikia malengo iliyojiwekea ikiwemo kufanikisha Mradi wa Kuendeleza Utalii Kusini (REGROW) ambao ni nguzo muhimu ya kunyanyua sekta ya Utalii kwenye mikoa ya Morogoro, Iringa, Njombe na Mbeya.

Vilevile Dkt. Abbasi ameongeza kuwa Wizara ya Maliasili iko mbioni kuanzisha Tuzo za Kisekta ambazo watapewa wadau wa utalii na uhifadhi waliofanya vizuri ili kuongeza msukumo katika kukuza sekta ya utalii na Uhifadhi kwa maendeleo endelevu ya nchi.

Nae Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Najma Giga ameipongeza Wizara ya Maliasili na Utalii na Taasisi zake kwa kutekeleza majukumu yake kwa uzalendo ambapo amesema licha ya kuwa na changamoto za kibajeti, imeweza kufikia malengo ya msingi kama yalivyopangwa.

Kikao cha Kamati ya Bunge kilihudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa wizara pamoja na watendaji kutoka katika Mradi wa uendelezaji utalii Kusini (REGROW).

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter