Home KILIMOKILIMO UFUNDI Rais Samia aagiza uzalishaji mbegu bora, bei ya mkulima

Rais Samia aagiza uzalishaji mbegu bora, bei ya mkulima

0 comments 193 views

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema ameshaiagiza Wakala wa Mbegu nchini (ASA) kuzalisha mbegu zenye ubora kwa bei ambayo mkulima ataimudu.

Rais Samia amesema lengo ni kujidhatiti kuzalisha mbegu za mazao yote hapa nchini ili kuachana na utaratibu wa kuagiza kutoka nje ya nchi.

Rasi Samia amesema hayo Oktoba 17, 2023 wakati akihutubia wananchi wa Nzega katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Samora.

Awali, Rais Samia aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) cha Wilaya ya Igunga ambacho kimegharimu Sh bilioni 2.6.

Amesema chuo cha VETA ni mwendelezo wa jitihada za serikali kuhakikisha vijana wanapata elimu ya ufundi itakayowasaidia kuajiriwa au kujiajiri.

“Serikali imeamua kujenga chuo cha ufundi stadi katika kila Wilaya nchini na kuwa na chuo kikubwa kimoja katika kila mkoa,” amesema Rais.

Amebainisha kuwa serikali imedhamiria kukuza ujuzi wa vijana kwani ndio nguvu kazi ya taifa hivyo vyuo vya VETA vinajengwa ili ziungane na miradi na mipango inayoanzishwa na serikali ili kujenga uchumi wa nchi.

Rais Samia ameanza ziara ya kikazi mkoani Tabora ambapo atafungua mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria kwa ajili ya mji wa Shelui, kupokea taaarifa ya mradi wa umeme vijijini (REA) awamu ya 3 mzunguko wa 2 na kuzungumza na wananchi wilaya ya Iramba.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter

Subscribe my Newsletter for new blog posts, tips & new photos. Let's stay updated!