Home KILIMO Walima ufuta wapewa somo

Walima ufuta wapewa somo

0 comment 56 views

Mwenyekiti wa Chama kikuu cha ushirika cha Runali, ambacho kinaundwa na wilaya za Nachingwea, Ruangwa na Liwale mkoani Lindi Hassan Mpako ametoa wito kwa wakulima wa ufuta katika wilaya hizo kuepuka kuuza zao hilo kwa wafanyabiashara kiholela na badala yake, wapeleke mavuno yao katika vyama vya ushirika ili kilimo hicho kiwanufaishe.

 

Mpako amesema kuwa, serikali imetangaza zao hilo linapaswa kununuliwa kwa mfumo wa stakabadhi ghalani kuanzia msimu huu ili kuwasaidia wakulima kuuza kwa bei nzuri na kuepuka wafanyabiashara wasio waaaminufu.

 

Kwa mujibu wa maelezo ya Mwenyekiti huyo, Chama cha Runali hivi sasa kinaendesha minada ya ununuzi wa ufuta ambapo kilo moja ya zao hilo huuzwa kuanzia Sh. 2,960 na wadau wengi wa kilimo hicho hasa wakulima wenyewe wameonyehwa kufurahishwa na mfumo huo wa ukusanyaji na mauzo na wameipongeza serikali kwa kuchukua hatua hiyo.

 

Mpako amewashauri wakulima kupeleka bidhaa zao moja kwa moja kwenye vyama vya ushirika na kuepuka kuuza bila mpangilio maalum kwani wanachoambulia ni kidogo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter