Home VIWANDA Mpango wa ASDP-11 waikosha SIDO

Mpango wa ASDP-11 waikosha SIDO

0 comment 33 views

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la kuhudumia viwanda vidogo nchini (SIDO) Prof. Sylvester Mpanduji amesema mbali na kuchochea uzalishaji zaidi wa chakula, Mpango wa Awamu ya Pili ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP 11) pia utasukuma ukuaji katika sekta ya viwanda na kufanikisha azma ya Rais John Magufuli ya kujenga uchumi wa kati na wa viwanda kufikia mwaka 2025.

“Mpango huu ni mzuri na umekuja wakati serikali imejipanga kujenga uchumi wa wakati, jumuishi na viwanda. Mafanikio ya utekelezaji wake yatasaidia sana maendeleo ya viwanda hapa nchini”. Amesema Prof. Mpanduji.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo, sekta ya viwanda haiwezi kusonga mbele bila malighafi yanayotokana na uzalishaji kwenye kilimo, mifugo na uvuvi na kusisitiza kuwa, sekta hizo zina mchango mkubwa katika kuleta mageuzi ya viwanda.

“Sisi kama SIDO tunaunga mkono mpango huu wa ASDP 11 kwani viwanda vidogo ni miongoni mwa wadau wakubwa wa mpango huo. Pamoja na kuhamasisha watanzania kushiriki katika ujenzi wa viwanda vidogo bado wana nafasi ya kufanikisha utekelezaji wa mpango huo”. Ameeleza Prof. Mpanduji.

Mkurugenzi huyo amesisitiza maendeleo endelevu ya viwanda yanatokana na uzalishaji mkubwa katika kilimo huku akiongeza kuwa, Tanzania ina fursa nyingi katika uwekezaji wa sekta hiyo na uhamasishaji zaidi unahitajika.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter