Home VIWANDANISHATI Majaliwa azindua umeme Lindi

Majaliwa azindua umeme Lindi

0 comment 30 views

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameagiza wakurugenzi wa halmashauri nchini kuhakikisha umeme unafika kwenye vituo vinavyotoa huduma kwa jamii kama vile hospitali na shule. Majaliwa amesema hayo baada ya kuzindua kituo cha kuunganisha umeme wa gridi ya taifa katika kijiji cha Mahumbika mkoani Lindi.

Majaliwa ameeleza kuwa lengo la Rais john Magufuli ni kuwawezesha watanzania kutumia umeme kufanya biashara mbalimbali zikiwemo vinywaji baridi pamoja na saluni ili kukuza uchumi wa taifa. Mbali na hayo, Waziri Mkuu pia ametoa wito kwa wakazi wa mkoa huo kulinda miundombinu ya umeme ili mradi hiyo iwe endelevu na itumike kusaidia jamii.

Kwa upande wake, Mkuu wa mkoa wa Lindi Erasto Zambi amesema uzinduzi wa mradi huo wa umeme ni wa kihistoria na ni hatua kubwa ya maendeleo katika mikoa ya Lindi ya Mtwara.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter