Home VIWANDA TADB kufufua kiwanda cha chai Kilolo

TADB kufufua kiwanda cha chai Kilolo

0 comment 118 views

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Japhet Justine amesema benki hiyo imekutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa wilaya ya Kilolo mkoani Iringa ambapo wamejadili uwezekano wa kufufua kiwanda cha kuchakata chai ili kuongeza uzalishaji wa zao hilo. Justine amefafanua kuwa wanalenga kuleta mapinduzi katika sekta ya kilimo ili kuwainua wakulima wadogo na wakubwa kutoka wilayani humo. Justine amesisitiza kuwa ni muhimu sana kufanya hivyo ili wakulima hao waweze kushirikiana na benki hiyo mpaka watakapoweza kusimama wenyewe pasipo msaada wowote.

“Kilimo ni uti wa mgongo wa taifa letu. Suala kama hili linalowanufaisha wakulima wetu, hivyo ni jukumu letu kuhakikisha wakulima wanapata msaada ambao utawawezesha kujiendeleza katika kilimo na kuinua uchumi wa taifa”. Amesema Kaimu huyo.

Vilevile katika maongezi yao, viongozi hao wamejadili kuhusu uanzishwaji wa kiwanda cha kuchakata chai ili kuhakikisha bidhaa ndogo kama majani ya chai yanatengenezwa nchini kwa ubora wa hali ya juu na kutumiwa ndani na nje ya nchi.

“Kuwepo kwa kiwanda hicho itakuwa moja ya njia ya kuunga mkono azma ya serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli ya kujenga uchumi wa kati na viwanda ifikapo mwaka 2025 kwa vitendo”. Amesema Justine.

Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya ya Kalolo Asia Abdalla ametoa pongezi kwa uongozi wa benki ya TADB kwa jitihada zao za kuisogeza benki hiyo karibu na wakulima.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter