Home HABARI ZA AFRIKA MASHARIKI Mradi wa bomba la mafuta kujadiliwa

Mradi wa bomba la mafuta kujadiliwa

0 comment 58 views

Mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Uganda kuja Tanzania ni moja ya ajenda zitakazojadiliwa katika mkutano mkuu wa kimataifa wa mafuta na gesi utakaofanyika jijini Dar es salaam kuanzia tarehe 24-25 Septemba mwaka huu.

Akiongea na waandishi wa habari kuhusu mkutano huo Abdulsamad Abdulrahim ambaye ni Mwanzilishi na Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa watoa huduma za mafuta na gesi nchini Tanzania (ATOGS) alisema mkutano huo licha ya kushirikisha serikali na wadau mbalimbali wa mafuta na gesi kama vile Shirika la maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na mengine kama vile PURA, EWURA, NEEC, ATOGS na TPSF pia mawaziri wa mafuta na gesi kutoka nchi mbalimbali za Afrika pia watashiriki.

Mkutano huo ambao utafanyika nchi kwa mara ya pili umeandaliwa na Pietro Fiorentini Tanzania kwa kushirikiana na CWC Group pamoja na serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini. Kupitia mkutano huo fursa mbalimbali za uwekezaji hasa katika miradi ya gesi na mafuta zitajadiliwa na itakuwa ni fursa kwa watoa huduma katika sekta hiyo nchini kukutana na wenzao wa kimataifa.

Licha ya fursa hizo mkutano huo unatajwa kuwa chachu ya kutambua fursa mbadala kama vile ajira,ushirikiano wa wadau wa ndani na nje pamoja na serikali katika kuendeleza miradi hiyo pia fursa za maswali yatakayojibiwa papo kwa papo itatolewa.

Mkutano huo na waandishi wa habari pia ulihudhuriwa na Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) Mhandisi Kapuulya Musomba pamoja na Kamishna Msaidizi wa Maendeleo ya Petroli kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Joyce Kisamo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter