• Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI
Wednesday, August 17, 2022
  • Login
  • Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI
No Result
View All Result
Pesatu
  • Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI
No Result
View All Result
Pesatu
No Result
View All Result

Serikali yataka ubunifu wa Watanzania ulindwe

Ubunifu ulindwe na kuendelezwa: Naibu Waziri Exaud Kigahe

Pesatu Reporter by Pesatu Reporter
August 12, 2022
in UWEKEZAJI
0
Picha| Mtandao

Picha| Mtandao

Share on FacebookShare on Twitter

Serikali kupitia Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara imetaka ubunifu wa Watanzania ulindwe na kuendelezwa.

Naibu Waziri wa Wizara hiyo Exaud Silaoneka Kigahe amesema vijana wengi Watanzania wana ubunifu lakini bunifu hizo huchukuliwa na watu wengine kutokana na kutolindwa kisheria.

Ameeleza kupitia taasisi za Wizara ambazo ni Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (Tanzania Industrial Research Development Organization – TIRDO) ambao wanasaidia wabunifu, pamoja na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Business Registrations and Licensing Agency – BRELA) ambao wanasajili makampuni mbalimbali lakini pia kulinda bunifu mbalimbali itahakikisha bunifu za Watanzania zinalindwa.

ADVERTISEMENT

“Tunafikiri sasa tuanze kulinda bunifu miliki za vijana wetu sababu wengi wa vijana wana ubunifu lakini sera zetu kidogo bado hazijawaona ili kufaidika na ubunifu huo,” amebainisha Naibu Waziri katika Mkutano wa Nishati (Tanzania Energy Congress) jijini Dar es Salaam.

Aidha, amesema Wizara inahamasisha kuona Watanzania wanaingia au kuchangia uzalishaji na uongezaji wa thamani katika bidhaa mbalimbali ikiwemo kwenye mazao ya kilimo.

“Kupitia Taasisi zetu ambazo ni za kiteknolojia na kushirikiana na Taasisi za ubunifu, tunataka kuona namna ya kuwawezesha wawekezaji na wajasiriamali wa Tanzania ambao wana fursa kubwa zaidi ya kufaidi rasilimali tulizonazo kwenye sehemu ya nishati.

Kwa sasa tunahamasisha kwenye nishati jadilifu (renewable energy) ambapo tunalenga zaidi kwenye solar na umeme wa upepo na kurejelesha taka (recycle) kuweza kuzalisha nishati,” amesema.

Ameeleza kuwa ili Watanzania waweze kufanikiwa katika hilo ni lazma Serikali iwawezeshe kimtaji na sera madhubuti.

“Sisi kama Wizara tunapitia sera yetu ya uwekezaji lakini pia sera zingine zinazohusiana na ujasiriamali.

Moja ya sera tunayotaka tuiunde sasa ni sera ya ubora (Quality Policy).

Hii inalenga kuona tutawezaje kuzalisha bidhaa ambazo zitakuwa na ubora kushindana na bidhaa nyingine kwa maana hata katika uzalishaji wa nishati tuweze kuwa shindani badala ya kuwasaidia tuu wawekezaji kutoka nje tuweza pia kuwasaidia wa ndani waweze kufaidika na rasilimali tulizonazo kama nchi.”

Tags: nishatiTanzaniaubunifuuwekezajivijana
Pesatu Reporter

Pesatu Reporter

Next Post

Bilioni 3 kujenga kiwanda cha parachichi Iringa

Discussion about this post

Habari Mpya

Filamu ya the hidden Tanzania inakuja: Rais Samia

August 15, 2022
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemiah Mchechu. Picha|Mtandao.

Wawekezaji wadau wakubwa ustawi wa uchumi: NHC

August 13, 2022

Bilioni 3 kujenga kiwanda cha parachichi Iringa

August 12, 2022
Picha| Mtandao

Serikali yataka ubunifu wa Watanzania ulindwe

August 12, 2022

Pato la utalii kupaa

August 5, 2022

Wakulima tumieni mitandao kujikwamua kiuchumi: TCRA

August 2, 2022

KUHUSU SISI

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905. PesaTu inamlenga kila mtu ambaye kwa namna moja au nyingine anaguswa na anapenda kujua/ kufuatilia masuala mbalimbali ya kiuchumi ya nchi ikiwemo ujasiriamali, uwekezaji, viwanda, kilimo na hisa.

LATEST

Filamu ya the hidden Tanzania inakuja: Rais Samia

by Pesatu Reporter
August 15, 2022
0

Rais wa Tanzania Samia Suhulu Hassan amesema awamu ya pili ya filamu ya kuonesha utalii wa Tanzania inakuja. Rais Samia...

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemiah Mchechu. Picha|Mtandao.

Wawekezaji wadau wakubwa ustawi wa uchumi: NHC

by Pesatu Reporter
August 13, 2022
0

Wawekezaji wametajwa kuwa moja ya wadau muhimu kwa ustawi bora wa uchumi wa Tanzania na kufungua fursa za ajira kwa...

RECOMMENDED

Waziri Mwijange aja na orodha ya viwanda visivyofanya kazi

by Patricia Richard
March 23, 2018
0

  Na Mwandishi wetu. Baada ya Rais John Magufuli kuonyesha kukerwa na kitendo cha Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji...

Nane Nane itumike kama darasa huru kwa wakulima

by Patricia Richard
March 23, 2018
0

Na Mwandishi wetu Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imejitolea kuwapa mafunzo ya siku moja wakulima mkoani Lindi...

No Result
View All Result
  • Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI

© 2022 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In