Home BIASHARAUWEKEZAJI Ukosefu wa mitaji watajwa changamoto inayowakabili wachimbaji wadogo

Ukosefu wa mitaji watajwa changamoto inayowakabili wachimbaji wadogo

0 comment 131 views

Kukosekana kwa mitaji kumetajwa kuwa miongoni mwa changamoto inayowakabili wachimbaji wadogo wa madini katika mgodi wa Mawe wa Ndolela Quarry uliopo kijiji cha Ndolela jimbo la Isimani mkoani Iringa.

Mwenyekiti wa Wachimbaji Mkoa wa Iringa ambaye pia ni miongoni mwa wamiliki wa mgodi wa Konga, uliopo kijiji cha Itengulinyi, mkoani Iringa Ibrahim Msigwa amesema ameitaja changamoto hiyo kuwa ni kubwa miongoni mwa wachimbaji wadogo.

“Tunawakaribisha wawekezaji wakubwa waje tushirikiane dhahabu zipo tushirikiane ili tuweze kuvuna, changamoto kubwa kwetu ni mitaji midogo,” amesema.

Mchimbaji mdogo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mgodi wa Madini ya Shaba Matembo, Elias Kazikuboma amesema changamoto kubwa ipo kwenye vifaa vya uchimbaji ingawa soko la uhakika la madini ya shaba lipo.

Ameeleza kuwa mgodi huo mchanga umekuwa ukitoa huduma mbali mbali za kijamii kama ujenzi wa matundu ya vyoo pamoja na vifaa mbalimbali.

Wachimbaji wadogo wakiwa kwenye shughuli zao.

Mgodi huo umeanza ujenzi wa Zahanati kwa kushirikiana na wananchi ambayo itaondoa adha ya wananchi hao kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya.

Mwenyekiti Mtendaji wa Kijiji cha Ndolela, Majuto Dumicus amesema Zahanati hiyo ikikamilika itaweza kuhudumia Kaya 377 zilizopo katika eneo hilo.

Amesema, ujenzi wa Zahanati hiyo ni kutimiza takwa la kisheria na Kanuni za Wajibu wa Wamiliki wa Leseni za Madini Kwa Jamii.

Kwa upande wa Meneja Msaidizi wa Mgodi wa Mawe wa Ndolela (Ndolela Quarry) Hilter Ranjiti amesema tangu kuanzishwa kwa mgodi huo mwaka 2022 umekuwa na manufaa kwa wananchi kwa kutoa ajira pia kutekeleza takwa la kisheria kwa kuchangia miradi ya maendeleo.

“Mgodi huu umekuwa na faida kwa wakazi wa Iringa, miradi mbali mbali ya Serikali tumekuwa tukichangia, umerahisisha pia upatikanaji wa kokoto mkoani Iringa siku za nyuma walifuata Lugoba au Dodoma,”amesema Ranjiti.

Aidha amesema, mgodi huo upo kwenye ujenzi wa Zahanati ya kijiji cha Ndolela na pia wamechangia marekebisho ya barabara ya Dodoma- Iringa.

Wachimbaji wadogo wakiwa kwenye shughuli zao.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter