Home VIWANDA Viwanda kuhamasishwa vijijini

Viwanda kuhamasishwa vijijini

0 comment 105 views

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Stella Manyanya amesema Wizara hiyo inashirikiana na Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) kuandaa michakato ambayo itasaidia kutumia rasilimali zilizopo katika kila kijiji nchini ili kuhakikisha nchi ina viwanda vya kutosha.

Manyanya ameyasema hayo wakati wa mkutano wa kuangalia changamoto za uwekezaji kati ya Tanzania na China uliofanyika jijini Dar es salaam ambapo ameeleza kuwa, Wizara hiyo inaendelea kusimamia ujenzi wa viwanda 100 katika kila mkoa, lengo likiwa ni kufika uchumi wa kati itakapofika mwaka 2025.

Licha ya Wizara hiyo kujikita katika kurejesha viwanda vyote vilivyochukuliwa na wawekezaji na kutoendelezwa akitoa mfano kiwanda kiongozi mstaafu aliyetajwa hivi karibuni na Rais Magufuli, Naibu huyo ametoa wito kwa waliopo vijijini kuhakikisha wanaanzisha viwanda na kuvikuza ili kuleta maendeleo.

“Ni lazima akirejeshe kwani ile ni amri na kama alikopa fedha kutumia kiwanda hicho na kuwekeza katika masuala mengine, atachukuliwa hatua za kinidhamu ikiwa ni pamoja na kufikishwa katika mahakama ya mafisadi” amesema Manyanya.

Hadi sasa sekta ya viwanda inachangia katika Pato la Ndani la Taifa (GDP) kwa asilimia nane na Wizara hiyo imejipanga kuchangia zaidi hadi kufikia mwaka 2025.

 

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter