Home BENKI KCB yatoa somo la kodi Arusha

KCB yatoa somo la kodi Arusha

0 comment 98 views

Benki ya KCB imeandaa kongamano kwa ajili ya kuwaelimisha wadau na wafanyabiashara kuhusu namna ya kusimamia fedha pamoja na jinsi ya kuendesha biashara na Sheria zinazohusu masuala ya kodi jijini Arusha.

Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa benki hiyo, Christine Manyenye, amesema moja ya malengo ya kongamano hilo ni kuzileta pamoja Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili taasisi hiyo iweze kupata elimu ya kutosha kutoka TRA na kuweza kufikia muafaka njia za kuweza kutatua changamoto ambazo taasisi hiyo imekuwa ikizipata ili kuchangia zaidi katika pato la taifa.

Meneja wa KCB Arusha, Judith Lubuva ametoa pongezi kwa wote waliohudhuria kongamano hilo na kusema kutokana na maendeleo makubwa katika sekta ya utalii, mkutano huo ni muhimu ili kupata mawazo mapya ya kuikuza zaidi sekta hiyo na kukuza uchumi wa nchi.

Kwa upande wake mwakilishi wa TRA, Ombeni Urio, amefurahishwa na maandalizi yaliyofanywa na KCB na kuwataka wafanyabiashara waliohudhulia kongamano hilo kufuata Sheria na kanuni za kodi ili kuepuka usumbufu katika biashara zao.

Wateja wapatao benki hiyo 250 wamehudhuria kongamano hilo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter