Home KILIMO Korosho Pwani kuanza kununuliwa wiki ijayo

Korosho Pwani kuanza kununuliwa wiki ijayo

0 comment 42 views

Mkuu  wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo amevitaka vyama vya ushirika vilivyopo mkoani humu kuhakikisha wanaziondoa korosho katika maghala yao ndani ya siku nne na kuzipeleka katika maghala makuu matatu yaliyoelekezwa na serikali likiwamo la Kibiti, Mkuranga na Tanita kabla hazijaanza kununuliwa wiki ijayo. Ndikilo amesema hayo alipozungumza na viongozi wa idara za mkoa na wilaya baada ya kutembelea ghala la kuhifadhi korosho na kiwanda cha kubangulia zao hilo ambapo amesema hatua hiyo ni mchakato wa serikali kuanza kununua korosho kwa njia rahisi na salama ili kuhakikisha wakulima wa zao hilo wanapata stahiki kama ilivyoagizwa na Rais Magufuli.

“Wenzetu Mtwara, Lindi na Ruvuma tayari wanaendelea kuuza korosho kama ambavyo mnasikia, lakini kwa upande wa Pwani tunaanza kununua korosho wiki ijayo kwa hiyo ili kuleta urahisi lazima korosho hizo zipelekwe katika maghala makuu matatu yaliyopangwa na serikali”. Amesema Ndikilo.

Mara baada ya korosho hizo kukusanywa katika maghala, Mkuu huyo wa mkoa amesema zitapimwa na wataalamu kulingana na mwongozo wa serikali na baada ya hapo, mkulima atalipwa bila usumbufu na baadaye magari ya jeshi yatakuja kuzisomba korosho hizo kama inavyofanyika Mtwara.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter